Sean Connery: Muigizaji wa filamu ya James Bond afariki dunia akiwa na miaka 90

0

WASHINGTON, MAREKANI 

SIR Sean Connery, muigizajiwa sinema ya James Bond amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90, familia yake imethibitisha.

Muigizaji huyo wa Uskochi alifahamika sana kwa kuwa mhusika wa katika sinema ya James Bond, na alikuwa wa kwanza kuleta sinema hiyo katika ukumbi wa sinema.

Sir Sean alifariki akiwa usingizini, akiwa Bahamas ambako amekuwa “akiugua kwa muda”, mwanawe wa kiume anasema.

Kazi yake ya uigizaji wa miongo mitano ilimwezesha kushinda tuzo ya Oscar mwaka 1988 kutokana na jukumu lake katika ‘The Untouchable’.

Filamu zingine alizoigiza Sir Sean ni pamoja na The Hunt for Red October, Highlander, Indiana Jones na the Last Crusade and The Rock.

Jason Connery, anasema baba yake “alikuwa na sehemu kubwa ya familia yake Bahamas ambayo ilikuwa naye” alipofariki usiku mjini Nassau.

Anasema: “Sote tunajaribu kukubaliana na msiba huu mkubwa kwani limetokea sasa, ingawa baba yangu amekuwa mgonjwa kwa muda.

“Ni siku ya huzuni kwa watu wote waliomfahamu baba yetu mpendwa na watu wote waliovutiiwa na uigizaji wake kote duniani.”

Sir Sean, anayetokea Fountainbridge, Edinburgh aliigiza filamu ya first James Bond mwaka 1962 na kuendelea mbele na kuigiza filamu zingine tano rasmi – na zingine ambayo sio rasmi kama vile Never Say Never Again mwaka 1983.

Aliamminiwa na watu wengi kuwa muigizaji mahiri ambaye ailiigiza 007 kwa muda mrefu, akiitwa majina hayo.

Alikabidhiwa tuzo ya knigh na Malikia Elizabeth katika eneo la Holyrood Palace mwaka 2000.

Mwezi Augosti, alisherehekea mwaka wa 90 wa siku yake ya kuzaliwa.

Aliunga mkono kwa muda mrefu uhuru wa Uskochi, akisema hayo katika mahojiano kuelekea kura ya maoni ya mwaka 2014 na kugusia kwamba huenda akarejea nyumbani kutoka Bahamas na kuishi Scotland enadapo itapiga kura kujitenga na Uingereza.

Waziri wa Kwanza wa Scotland Nicola Sturgeon anasema: “Nimevunjika moyo kupokea taarifa za kifo cha Sir Sean Connery. taifa letu linaomboleza kwa kumpoteza mpendwa wetu.

Sir Thomas Sean Connery amezaliwa Agosti 25, 1930 pia inasemekana kazaliwa 1922 ni mwigizaji na mtaarisha wa filamu mstaafu kutoka nchini Scotland, ambaye huenda akawa anafahamika kama mwigizaji wa kwanza kuigiza katika mfululizo wa filamu za James Bond, aliyecheza katika filamu sita.

Mnamo mwaka wa 1987 na ameshinda tuzo hiyo ya Oscar kama mwigizaji msaidizi kutoka katika filamu ya The Untouchables. Mwaka wa 2000 amepewa cheo cha “Sir” cha Uingereza.

Walioigiza filamu za James Bond

Waigizaji waliocheza kama 007 katika mfululizo rasmi wa filamu
Sean Connery • George Lazenby • Roger Moore • Timothy Dalton • Pierce Brosnan • Daniel Craig
Wengine waliocheza kama 007
Barry Nelson • Bob Holness • David Niven • Sean Connery • Maxwell Caulfield • Adam Blackwood • Tim Bentinck • Jason Carter • David Houston • Toby Stephens
Washiriki wengine waliocheza katika filamu za James Bond ni wasichana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here