Sasa naweza kuwaalika tukala meza moja-Lewandowski adai yupo levo moja na Messi, Ronaldo

0

BERLIN, UJERUMANI

BAADA ya Robert Lewandowski kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa FIFA na kuwapiku Lionel Messi na Cristiano Ronaldo amedai kuwa anahisi yupo katika levo moja na wachezaji hao na sasa anaweza kuwaalika na kupata kula chakula pamoja. Mshambuliaji huyo wa klabu ya Bayern Munich ameyasema hayo katika mahojiano na France Football ambapo pia aligusia namna yeye alivyonukia kutua United mwanzoni mwa kusakata kwake mchezo wa soka alipokuwa swali la mwandishi. Mshambuliaji huyo wa klabu ya Bayern Munich ameyasema hayo katika mahojiano na France Football ambapo pia aligusia namna yeye alivyonukia kutua United mwanzoni mwa kusakata kwake mchezo wa soka alipokuwa swali la mwandishi. Miaka miwili iliyopita mchezaji wa Barcelona, Antoine Griezmann aliwahi kusema kwa kujilinganisha kuwa meza moja na Messi na Ronaldo katika uwezo. Lewandowski ametumia njia hiyo hiyo na yeye kujilinganisha na wachezaji hao wafalme wa soka kwa sasa duniani.

Wakati huo huo, Mshambuliaji huyo wa klabu ya Bayern Munich Robert Lewandowski amesema kuwa ilikuwa bado kidogo tu yeye kujiunga na Mashetani wekundu Manchester United mwaka 2012 wakati wa kocha Sir Alex Ferguson.

Mchezaji huyo wa Poland mwenye umri wa miaka 32 amesema alifurahia mno msimu mzuri aliyokuwa akiitumikia Borussia Dortmund miaka kumi iliyopita.

Hata hivyo amesema United ilionyesha nia ya kumuhitaji na kuanza kushawishika zaidi ikiwa chini ya Ferguson ambaye alimfuata mwenyewe Lewandowsk kuzungumzia usajili wake.

Akizungumza wiki hii na France Football baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa FIFA kwa mwaka huu wa 2020, Lewandowski amedai United ilikuwa imeanza mipango ya kukamilisha mpango huo. ”Baada ya mwaka wangu wa pili Dortmund, nilianza mazungumzo na Sir Alex Ferguson, alihitaji mimi niende Manchester,” amesema Lewandowski.

”Nilivutiwa sana, ningeweza kusema hata nipo tayari, lakini Dortmund hawakuwa tayari kuniacha niende, hata hivyo hatua hiyo haikunikasirisha kwa sababu mambo yalikuwa yanakwenda vizuri Borussia.”

Dortmund kusita kumuuza mshambuliaji huyo na kusalia chini ya kocha Jurgen Klopp kulipelekea baadaye kuondoka kama mchezaji huru na kujiunga na Bayern Munich.

Ferguson alifanya mawasiliano na Lewandowski mwaka 2012, kabla muda wake wa kuondoka Man United ambapo baada ya kumkosa Mpoland huyo ndipo akaletwa Robin van Persie akitokea Arsenal.

 

Hivi karibuni mchezaji huyo, Lewandowski alishinda tuzo kubwa kabisa ya taaluma yake, na kudhihirisha kuwa mshambuliaji ambaye sio Messi au Ronaldo anaweza kupigiwa kura ya kuwa mchezaji bora wa kandanda duniani.

Nahodha huyo wa Poland ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA Mwanaume katika mwaka wa 2020 baada ya mabao yake 55 ya msimu kuisaidia Bayern Munich kunyakua mataji ya kimataifa na ya nyumbani.

Lewandowski alipata kura 52 dhidi ya 38 alizopata Lionel Messi wakati Cristiano Ronaldo akipata 35. Hafla ya tuzo hiyo ilifanyika Zurich kwa njia ya video lakini Rais wa FIFA Gianni Infantino alikwenda hadi Munich kumkabidhi binafsi Lewandowski tuzo yake. Lucy Bronze wa Uingereza alishinda tuzo hiyo kwa upande wa wanawake.

Alishinda Ligi ya Mabingwa akiwa na Olympique Lyonnais kabla ya kuhamia Manchester City. Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alimpiku Mjerumani mwenzake Hansi Flick wa Bayern Munich na Marcelo Bielsa wa Leeds katika tuzo ya kocha bora. Manuel Neuer alishinda tuzo ya kipa bora.

afp, dpa,reuters, dpa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here