Samia awatembelea majeruhi ajali ya treni

0

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewatembelea majeruhi wa ajali ya treni katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma ambapo ametoa maagizo kwa mkoa kuhakikisha wanasaidiwa kufika makwao mara watakapopata nafuu.

Samia alitoa kauli hiyo baada ya kuzunguka katika wodi zote walikolazwa majeruhi hao na kuzungumza nao lakini akasema ameridhishwa na hali zao pamoja na huduma wanayopata wagonjwa hao.

Kiongozi huyo amefika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma mapema saa moja asubuhi na mbali na kuzungumza na majeruhi wa treni lakini amezungumza na wagonjwa wengine akiwafariji.

“Nawaagiza uongozi wa Mkoa, Wizara ya afya na Shirika la reli mshirikiane kuona wagonjwa hawa wanapata huduma zote na itakapothibitika wanaweza kuruhusiwa, wasaidieni wafike makwao salama,” alisema Samia.


Akizungumzia hali za majeruhi, amesema wanaendelea vizuri isipokuwa wawili ambao walikuwa wamefanyiwa upasuaji katika miguu na mikono na mmoja alikuwa akilalamika maumivu ya kichwa lakini madaktari walisema hakuwa na maumivu wala mpasuko kichwani.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here