Sababu 3 zinazoonesha watu weusi hubaguliwa Marekani

0

NA MWANDISHI WETU

Hivi karibuni ghasia ziliibuka katika miji tofauti nchini Marekani kufuatia kifo cha George Floyd, raia wa nchi hiyo mwenye asili ya kiafrika ambaye alikuwa amekamatwa na polisi.

Tumeangalia baadhi ya data zinazoangazia hali ya uhalifu na haki nchini Marekani, kubaini zinasema nini kuhusu maisha ya Wamarekani weusi linapokuja suala la utekelezaji wa haki na sheria.

  1. Wamarekani weusi wako katika hatari ya kuuawa kwa kupigwa risasi

Takwimu zilizopo zinaonesha katika visa ambapo polisi wamepiga risasi na kuua, idadi ya Wamarekani weusi inakadiriwa kuwa juu ikilinganishwa na watu wa jamii zingine nchini Marekani.

Inasadikiwa kuwa, mwaka 2019, japo Wamarekani weusi walichangia asilimia 14 ya idadi jumla ya watu nchini Marekani (kwa mujibu wa sensa rasmi), walikadiria zaidi ya asilimia 23 ya vifo 1,000 vilivyotokana na kupigwa risasi na polisi.

Na idadi hiyo imekuwa ikiongezeka tangu mwaka 2017, wakati idadi ya Wamarekani weupe walioathiriwa ikiendelea kupungua kutoka wakati huo

  1. Wamarekani weusi wengi wanakamatwa kwa utumizi wa dawa za kulevya

Idadi ya Wamarekani weusi wanaokamatwa kutokana na utumizi wa dawa za kulevya iko juu kuliko ya Wamarekani weupe, japo uchunguzi unaonesha viwango vya matumizi ya dawa za kulevya kati ya jamii hizi viko sawa.

Mwaka 2018, karibu watu 750 kati ya kila Wamarekani weusi 100,000 walikamatwa kwa kosa la utumizi wa dawa za kulevya, ikilinganishwa na karibu watu 350 kati ya kila Wamareekani weupe 100,000.

Tafiti zilizopita za kitaifa kuhusu utumizi wa mihadarati zinaonesha watu weupe wanatumia dawa za kulevya kwa viwango sawa, lakini Wamarekani weusi wanaendelea kukamatwa kwa kiwango kikubwa.

Kwa mfano, utafiti uliofanywa na Muungano wa Uhuru wa Raia wa Marekani, ulibaini kuwa Wamarekani weusi walikuwa katika hatari ya kukamatwa mara 3.7 wakipatikana na bangi ikilinganishwa na Wamarekani weupe, japo matumizi yao ya bangi ni sawa.

  1. Wamarekani weusi wanafungwa zaidi

Wamarekani wenye asili ya Kiafrika wanakabiliwa na tishio la kufungwa mara tano zaidi ikilinganishwa na Wamarekani weupe mara miili zaidi ya Wamarekani wenye asili ya Kihispania, kwa mujibu wa data za hivi karibuni.

Mwaka 2018, Wamarekani weusi walikadiria 13% ya idadi ya watu Marekani, lakini karibu thuluthi moja ya idadi ya wafungwa nchini humo ni wao.

Wamarekani weupe wanakadiriwa kuwa karibu 30% ya wafungwa licha ya idadi yao kuwa zaidi ya 60% ya watu wote nchini Marekani.

Hii inamaanisha kuna zaidi ya wafungwa 1,000 kwa kila Wamarekani weusi 100,000, ikilinganishwa na wafungwa 200 kwa kila Wamarekani weupe 100,000

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here