Rose Ndauka sio muumini wa ‘make up’

0

Na Mwandishi Wetu

Muigizaji wa filamu nchini, Rose Ndauka amesema pamoja na jamii kubwa ya Watanzania kuamini mastaa wa kike hawawezi kufanya kazi zao bila kujiremba lakini kwa upande wake imekua tofauti.

Rose ambaye hivi karibuni alifunga ndoa alisema suala la kutumia gharama kubwa kujiremba kwake halipi kipambaumbele kwa kuwa mara nyingi amekua akiamini uzuri wa asili yake.

”Mimi sio muumuni sana wa make up, ipo dhana kwamba wasanii wa kike hawawezi kutoka majumbani mwao bila makeup, kwangu haipo hivyo, najiamini sana na uasilia wangu, hata wakati mwingine ninapokwenda kufanya kazi zangu za sanaa huwa napaka mafuta tu kisha nakwenda,” alisema Rose.

Katika hatua nyingine mwanadada huyo ambaye ni mama wa watoto wawili amefunguka kuwa kwa sasa anafurahia maisha yake ya ndoa na anaamini yupo kwenye mikono salama kwa mumewe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here