Roma Mkatoliki atangaza kuacha muziki

0

Na Bethsheba Wambura 

Msanii wa miondoko ya kufoka foka (Hip Hop), nchini Ibrahim Musa maarufu Roma Mkatoliki ametangaza kuacha kufanya sanaa hiyo aliyoifanya kwa miaka 13 huku akiwashukuru wote waliompa sapoti katika kipindi chote hicho.

Roma ametangaza nia yake hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter leo Jumanne Disemba 8, 2020.

“Wimbo wangu wa kwanza niliutoa mwaka 2007, wimbo wangu wa mwisho nitautoa muda wowote kuanzia sasa na huu ndio utakua wimbo wangu wa mwisho, asanteni kwa kuwa nami na kuni-support kwa kipindi chote cha miaka 13 niliyowahudumia kwenye sanaa hii ya muziki,” ameandika Roma ambaye yuko nje ya Tanzania kwa kipindi kirefu sasa.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here