REGROW; Mradi unaotekelezwa na Serikali kuongeza utalii kusini

0

NA JONAS MUSHI

AWAMU ya pili ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano 2016/17-2020/21 unaitambua sekta ya utalii kama njia ya uhakika ya kukuza uchumi kutokana na kuendelea kuongezeka kwa idadi ya watalii na mapato yatokanayo sekta hiyo.

Uchumi wa Tanzania unategemea zaidi maliasili ambazo nyingi zipo katika maeneo yaliyohifadhiwa yaliyoyotapakaa kote nchini.

Kwa mujibu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) hivi sasa maeneo ambayo yanapokea watalii wengi ambayo ni ukanda wa Kaskazini umeanza kuelemewa na wingi wa watalii kulinganisha na uwezo wake.

Inabainishwa kuwa miundombinu mingi ya utalii ipo kaskazini huku ile ya kusini ikiwa haitoshelezi na haipo katika hali nzuri.

Serikali kupitiwa Wizara ya Maliasili na Utalii inakusudia kuufanya ukanda wa kusini kuwa maarufu kwa utalii na hivyo kuufanya utalii kama njia ya kukuza uchumi wa maeneo hayo na Taifa kwa ujumla.

Utafiti uliofanywa na Serikali uliopewa jina la Mkakati wa Mendeleo ya Utalii Kusini mwa Tanzania ambao ulisimamiwa na mshauri Dalberg and Solimar Consultants, ulionyesha kuwa hifadhi za Udzungwa, Mikumi, Ruaha na Nyerere ni kitovu cha utalii kusini.

Utafiti ulionyesha kuwa maeneo hayo yana vitu vingi vinavyoweza kuinua utalii, kuongeza ajira pamoja na kuweza kuleta athari chanya kwa sekta zingine, kutengeneza ushoroba wa utalii kuunganisha na maeneo mengine yenye vivutio na utajiri mkubwa wa historian a utamaduni.

Pia utafiti huo pia ulionyesha kuwa Hifadhi nyingi zilizopo kusini hazifikiki kirahisi kutokana na miundombinu mibovu pamoja na kutokuwa na maeneo ya kuwatunza watalii. Ulianisha barabara mbovu, milango michache ya kuingilia, viwanja vya ndege vibovu, malazi yasyoridhisha, kutokuwepo kwa vituo ya taarifa kwa watalii, malazi yasiyotosheleza kwa wafanyakazi pamoja na vitendendea kazi.

Kutokana na hayo Serikali ilisaini kataba wa mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia wa Dola za Marekani milioni 150 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 300, kwaajili ya utekelezaji wa mradi wa kubadilisha sekta ya utalii kusini mwa Tanzania unaojulikana kama  “Resilient Natural Resources Management for Tourism and Growth (REGROW)”.

Lengo la mradi huo ni  ni kuimarisha usimamizi wa maliasili na miundombinu ya utalii katika maeneo maalumu kusini mwa Tanzania na kuongeza shughuli mbadala za jamii ambazo zinategemea maeneo ya hifadhi.

REGROW inajikita zaidi katika ushoroba wa kusini ambao una hifadhi za Ruaha, Udzungwa, Mikumi, Nyerere, Katavi, Kitulo, na  Mahale miongoni mwa vivutio vingine pamoja na mji wa Iringa ambao utakuwa kituo kikuu cha utalii kusini.

Mradi huo unatekelezwa kwa miaka sita ambao uliazna mwaka wa fedha 2017/18 lakini utekelezaji ulianza rasmi Machi 2019 na unatarajiwa kukamilika 2023.

Mradi wa REGROW unatekelezwa na Serikali chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii ambayo ndiyo waratibu wa mradi.

TANAPA kama miongoni mwa taasisis zinazotekeleza mradi huo inasimamia utekelezaji katika hifadhi nne za Ruaha, Udzungwa, Mikumi na Nyerere.

Taasisi zingine zinazotekeleza mradi huo ni pamoja na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ambayo inasimamia za kutangaza utalii. Wengine ni Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori  (TAWIRI) ambayo inaendesha shughuli za tafiti za wanayamapori.

Pia Baraza la Taifa la Umwagiliaji (NiRC) ambao wanaratibu  mafunzo kwa vitendo kwa wakulima na kuimarisha umwagiliaji wakishirikiana na Bonde la Rufiji.

Wengine ni Bodi ya Maji (RBWB) kwa shughuli zinazohusiana na ugawaji wa rasilimali maji na kusimamia maeneo oevu.

Wapo pia Taasisi ya Huduma za Misitu (TFS) ambao wanasimamia utekelezaji wa mradi katika maeneo ya misitu.
Mradi huo una vipengelevikuu vinne moja ikiwa ni kuimarisha usimamizi na uboreshaji wa miundominu katika maeneo ya hifadhi kwa upande wa TANAPA.

Mbili ni kuimarisha shghuli mbadala za jamii zinazozunguka hifadhi ili kupunguza utegemezi wao katika rasilimali zilizopo katika hifadhi.

Kipengele cha tatu ni kuimarisha usimamizi na miundombinu ya uwekezaji katika Hifadhi ya Ruaha na nne ni usimamizi wa mradi, kujenga uwezo wa taasisi, kudhibiti ubora pamoja na ufuatiliaji na tathmini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here