RC Ndikilo: Wawekezaji epukeni uhasama kati yenu

0

NA MWANDISHI WETU, KIBAHA

MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amesema Mkoa huo hauwezi kumvumilia mwekezaji yeyote atakaye kuwa kikwazo cha mwingine kukamilisha shughuli zake kwa wakati

Ndikilo alisema Serikali haiwezi kukubaliana na kitu chochote kinachokwamisha uwekezaji na juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano.

Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipotembea ujenzi wa kiwanda cha Wen xing Plastic kinachotarajia kuanza utengeneza viatu, ndoo na bidhaa za plastiki.

Ndikilo akiwa katika kiwanda hicho alisema hakuna haja ya wawekezaji kuwekeana uhasama badala yake wanatakiwa kushirikiana kwani wengi wao wanategemeana katika mahitaji mbali mbali.

Alitoa kauli hiyo baada ya kuwepo kwa mgogoro Kati ya wamiliki wa kiwanda hicho na Kampuni ya Saibaba ambayo ilikuwa ikibitaji Shilingi Milion 60 kwa madai ya kutoachwa nafasi kutoka Kiwanda hicho Cha plasitiki na ukuta wa eneo lao ambalo bado hawajliendeleza kwa miaka mitano sasa.

Alisema kutokuwa na mawasiliano mazuri Kati ya wawekezaji hao wawili ambao ni majirani haikua ikileta picha nzuri.

Ndikilo alimaliza mgogoro huo na kuwasihi wawekezaji hao kuwa na ushirikiano kila mmoja aweze kutimiza malengo yake ya kuwekeza ambapo aliwakafibisha katika Ofisi yake kujadili wanapoona kuna jambo linatakiwa kupatiwa ufumbuzi

 Awali meneja wa mradi Kantilal Laxman wa Kampuni ya Saibaba alimueleza mkuu wa Mkoa kuwa wamiliki wa kiwanda cha plasitiki hawakuzingatia nafasi wakati wa kujenga ukuta wao jambo ambalo ni la hatari pale litakapotokea janga la moto.

Alisema kutokana na hali hiyo Kampuni ya Saibaba ilienda kufikisha malalamiko hayo katika Halmashauri ya mji wa Kibaha na baadae ofisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili waweze kulipwa milion 60.

Hata hivyo baada ya Mkuu wa mkoa kuongea na wawekwzaji hao mgogoro buo ulimalizika na kila mmoja kuruhusiwa kuendelea na kazi zake.

Awali msemaji wa kiwanda cha plastiki Yoyo alisema kiwanda hicho kitakapokamilika kinatarajia kutoa ajira 500 .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here