RC KUNENGE AWAELEKEZA TARURA KUMBANA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI WA DARAJA LA ULONGONI ‘A’ NA ‘B’ KABLA YA MWEZI WA SITA

0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Daraja la Ulingoni A na B na kuwaelekeza TARURA kuhakikisha wanambana Mkandarasi aendelee kufanya kazi usiku na Mchana ili ifikapo mwezi wa Tano kazi iwe imekamilika na Daraja lianze kutumika mwezi wa Sita.

RC Kunenge ametaka kazi ya Ujenzi huo ifanyike ata wakati wa kipindi Cha Mvua sababu kwa sababu kazi ya kusimika nguzo ya katikati ipo hatua ya mwisho kukamilika hivyo anaamini mvua haiwezi Tena kukwamisha Ujenzi kuendelea.

Aidha RC Kunenge amesema kinachompa faraja ni kuona kazi inakwenda vizuri ndio maana ata ile Chuki waliyokuwanayo wananchi kipindi Cha kwanza zimeanza kupungua sababu kazi inaonekana.

Hata hivyo RC Kunenge amesema kinachofurahisha ni kwamba Ujenzi wa Daraja hilo unakwenda sambamba na ujenzi wa Barabara za lami na Ujenzi wa kingo za mto kwa lengo la kuzuia maji kuingia kwenye makazi ya watu na kusomba nyumba zao.

Kwa upande wake Mratibu wa TARURA Mkoa wa Dar es salaam Mhandisi Geoffrey Mkinga amesema Ujenzi wa Daraja la Ulingoni A Ujenzi umefikia 56 wakiwa nyuma kwa 03% lakini wamembana Mkandarasi aongeze kasi ya Ujenzi na kuahidi kuongeza watu ili kufidia hizo 03%.

Aidha kwa upande wa Daraja la Ulingoni B Mhandisi Mjinga amesema Ujenzi umefikia 62% na Mkandarasi anaendelea na ukamilishaji wa nguzo ya katikati ambayo ikikamilika itawezesha kufanyika kwa kazi ata mvua zikiwa zinanyesha na wanaamini kufikia mwezi wa tano Daraja litakabidhiwa na litaanza kutumika mwezi wa sita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here