RC Arusha akerwa na kusuasua kwa Ujenzi wa Vyuo vya VETA

0

Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Kimanta ameagiza kuharakishwa kwa ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi katika wilaya za Monduli na Longido mkoani Arusha ambapo pamoja na serikali kutoa zaidi ya shilingi bilioni 3.4 lakini ujenzi wake umekuwa ukisuasua.

Mkuu wa Mkoa Kimanta ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyuo hivyo ulioanza mwezi Februari mwaka huu na vilitakiwa viwe vimekamilika ndani ya miezi sita huku kila kituo kikipatiwa fedha zaidi ya shilingi bilioni 1.7.

Kimanta ameshangazwa na kusuasua kwa ujenzi wa vyuo hivyo vilivyopo katika eneo la Makuyuni kwa wilaya ya Monduli na katika mji wa Longido katika wilaya ya Longido huku vikitakiwa kuanza kuchukuwa vijana mapema mwaka ujao na akaagiza sehemu kubwa ya ujenzi iwe imekamilika ifikapo Disemba 31 mwaka huu.

Kwa upande wao mkuu wa wilaya ya Monduli kamishina msaidizi wa Polisi ACP Edward Balele,Mkuu wa chuo cha Ufundi Stadi Makuyuni Felix Ole Ndukai na Meneja wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) mkoa wa Arusha Mhandisi Herini Mhina wameahidi kuhakikisha ujenzi unafanyika kwa kasi.

Mkuu huyo wa mkoa mkoa pia ameitaka mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini (VETA) ambayo ndiyo inayovisimamia vyuo hivyo kushughulikia vikwazo vinavyokwamisha kukamilika kwa vyuo hivyo ambavyo vinavyokwamisha kukamilika kwa vyuo hivyo ambavyo vipo katika hatua ya upauaji kikiwemo cha aina ya rangi ya mabati yanayotakiwa pamoja na upatikanaji wa saruji).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here