Rais wa Belarus awekewa vikwazo na EU

0

BRUSSELS, UBELGIJI

UMOJA wa Ulaya umemuwekea vikwazo rais wa Belarus na maafisa wake 14 kwa kuhusika na ukandamizaji wa raia wakati wa maandamano ya kupinga uchaguzi wa rais uliofanywa mwezi Agosti.

Umoja wa Ulaya umesema katika taarifa yake kwamba, Rais wa Belarus Alexander Lukashenko,mtoto wake pamoja na mshauri wake wa usalama wa taifa, Viktor Lukashenko, wamewekwa kwenye orodha ya vikwazo hivyo.

Watakabiliwa na marufuku ya kusafiri ndani ya mataifa ya Umoja wa Ulaya na mali zao zitazuiwa. Aidha raia wote wa Ulaya pamoja na makampuni hawaruhusiwi kuwapatia mikopo.

Tangu mwezi Agosti kumekuwako maandamano ya raia kote nchini Belarus, na zaidi ya watu 15,000 wamekamatwa na polisi.

Raia wa Belarus pamoja na Umoja wa Ulaya wanadai kwamba matokeo ya uchaguzi yalikuwa na udanganyifu ambayo yalimpa Lukashenko ushindi wa urais kwa asilimia 80.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here