Rais wa Armenia agoma kumfukuza kazi mkuu wa majeshi

0

Rais wa Armenia, Armen Sarkissian amekataa kumfukuza kazi mkuu wa majeshi uamuzi unaozidisha mvutano baina ya Waziri Mkuu Nikol Pashinyan na jeshi, ambaye siku chache zilizopita alidai kuwa jeshi lilitaka kumpindua.

Siku ya Alhamis, Waziri huyo mkuu alimfuta kazi mkuu wa jeshi, lakini uamuzi huo ulihitaji kuidhinishwa na rais ambaye amekataa akisema ni kinyume na katiba na jeshi linapaswa kuwekwa kando na siasa.

Waziri Mkuu Pashinyan amekosoa hatua hiyo ya rais akisema uamuzi huo hautoi ufumbuzi kwa mgogoro unaoendelea nchini humo.

Jeshi lilimtaka waziri huyo mkuu kujiuzulu katika kile wakosoaji wanasema ni namna mbaya ya serikali yake ilivyoshughulikia mzozo baina ya Armenia na Azerbaijan juu ya mkoa wa Nagorno-Karabakh. Ilikuwa ni mara ya kwanza jeshi kutamka hadharani likimtaka Pashinyan kujiuzulu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here