Rais Ndayishimiye ampongeza Magufuli

0

Na Bethsheba Wambura

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye ametuma salamu za pongezi kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020.

Ndayishimiye ametuma pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo ameandika; “Kwa niaba ya Watu wa Burundi, na kwa niaba yangu binafsi kwa moyo mkunjufu nampongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa tena.

”Nawapongeza Watu wa Tanzania ambao waliamua maisha yao ya baadaye kwa amani na kuonyesha ukomavu wa kidemokrasia.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here