Rais Magufuli kuanza na haya

0

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Mara baada ya kuapishwa kuwa Rais kwa mhula wa pili, John Magufuli ametaja mambo kadhaa atakayoyafanya katika kipindi cha miaka mitano kuanzia leo Alhamisi Novemba 5, 2020.

Akizungumza katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma inakofanyika hafla hiyo na kuhudhuriwa na mamia ya watu wakiwemo viongozi wa kitaifa na kimataifa, Rais Magufuli ametaja usimamizi wa maliasili na rasilimali za nchi, kukuza uchumi  na kushughulika na changamoto za Watanzania ikiwemo ajira hasa kwa vijana.

Pia ametaja mapambano dhidi ya rushwa, wizi na ubadhirifu wa mali za umma.

Ameahidi kuendelea kushirikiana na Watanzania kwa karibu na kukamilisha miradi mbalimbali mikubwa na kuanzisha mingine mipya.

“Nitaendeleza usimamizi wa maliasili, madini rasilimali za baharini na majini, wanyamapori, mifugo na kadhalika, sambamba na hilo tutatekeleza kwa namna kubwa katika kukuza uchumi na kushughulikia changamoto za umasikini zinazowakabili Watanzania. Ukosefu wa  ajira kwa vijana na kero mbalimbali kwa wananchi.”

“Aidha tutazidisha mapambano dhidi ya rushwa, wizi, na ubadhirifu wa mali za umma,” amesisitiza kiongozi mkuu huyo wa nchi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here