Home Uncategorized Magufuli awatoa hofu Watanzania kuhusu Corona, ataka wachape kazi wakichukua tahadhari

Magufuli awatoa hofu Watanzania kuhusu Corona, ataka wachape kazi wakichukua tahadhari


Mwandishi Wetu

Rais Dk. John Magufuli amewataka Watanzania kutotishwa na janga la ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.

Amesema badala yake waendelee kuchapa kazi na kujenga uchumi huku wakizingatia tahadhari zote za kujikinga kuambukizwa ugonjwa huo kama zilivyotolewa na wataalamu.

Rais Magufuli amesema hayo leo Jumapili Machi 22, 2020 alipohudhuria Ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Paulo wa Msalaba Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma  iliyoongozwa na Paroko wa Parokia hiyo, Padri Onesmo Wisi.

Katika salamu zake katika Ibada hiyo, Magufuli amesema kuwepo kwa ugonjwa wa corona isiwe sababu ya kutishana kiasi cha kumsahau Mungu.

Ametoa wito kwa Wakristo na waumini wa madhehebu mengine kumrudia Mungu ili aepusha janga hili, badala ya kumwacha shetani atawale.

Rais Magufuli pia amekemea tabia za baadhi ya watu wanaofanya mzaha juu ya ugonjwa huu ama kuwatia hofu wananchi kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, na badala yake ametaka Watanzania waendelee kuchapa kazi huku wakizingatia tahadhari.

“Watu tusitishane, tunatishana mno. Niwaombe ndugu Wakristo na Watanzania kwa ujumla wa madhehebu yote, huu ndio wakati mzuri sana wa kumtegemea Mungu kuliko wakati wote.

“Tuendelee kuchapa kazi, tuendelee kuujenga uchumi wetu, hatuwezi kusalimu amri kwa ugonjwa huu wa Corona na kushindwa kumtegemea Mungu na tukashindwa kuendeleza uchumi wetu,” amesema Magufuli.

Aidha amewashukuru viongozi wa Dini kwa kuungana na Serikali katika kuwahamasisha wananchi kuchukua tahadhari na ametoa wito kwa viongozi hao kuendelea kuliombea Taifa ili Mungu aepushe ugonjwa huo uliosababisha vifo vya watu zaidi ya 13,000 duniani kote hadi jana saa 5 usiku.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -

Most Popular

Yanga yampatia Tshishimbi mkataba mpya

NA MWANDISHI WETU Klabu ya Yanga SC, imesema kuwa tayari imemaliza kazi yake ya kuhakikisha inambakiza kiungo tegemeo wa...

Tetesi za soka barani Ulaya

SANCHO AITIKISA UNITED Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Timu ya Taifa ya Uingereza, Jadon Sancho (20), amesema hatakuwa tayari...

Makonda: Wazururaji hawatakwenda mahabusu watazibua mitaro ya maji machafu

NA MWANDISHI WETU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuwa watu watakaokamatwa kwenye mkoa huo kutokana...

Chui katika hifadhi ya wanyama ya Bronx akutwa na Virusi vya Corona

NEW YORK, MAREKANI Chui wa kike wa Malaysia aliyefahamika kwa jina la Nadia mwenye umri wa miaka minne katika hifadhi...

Recent Comments