Rais Magufuli amteua Jaji Mwangesi kuwa Kamishna wa Maadili

0

Rais Dk. John Magufuli amemteua Sivangilwa Mwangesi ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani kuwa Kamishna wa Maadili.

Jaji Mwangesi ameteuliwa kushika wadhifa huo baada ya Jaji wa Mahakama ya Rufani Mstaafu, Harold Nsekela kufariki dunia Disemba 6, mwaka huu.

Katika taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, uteuzi  wa Jaji Mwangesi unaanza leo Disemba 23, 2020 na ataapishwa Disemba 24, 2020 Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here