Rais Kenyatta ampongeza Magufuli

0

Nairobi, Kenya

RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amemtumia salamu za pongezi kwa Rais Dk. John Magufuli kwa kushinda uchaguzi uliofanyika Oktoba 28.

Rais Kenyatta alisema kuchaguliwa tena kwa Magufuli ni ishara ya upendo na imani waliyo nayo Watanzania kwa uongozi wake.

“Kwa niaba ya watu, Serikali ya Kenya na mimi mwenyewe nampongeza ndugu yangu, Dk John Pombe Magufuli kwa ushindi wako na wa Chama Cha Mapinduzi, katika uchaguzi uliomalizika..

”Nchi ya Kenya inatarajia kuendelea kufanya kazi na utawala wako kwa faida ya watu wa mataifa yetu mawili, kwa ustawi wa Afrika Mashariki na kwa amani, utulivu na ukuaji wa Bara la Afrika,”alisema.

Rais Kenyatta pia amemtakia Rais Magufuli afya njema na ufanisi anapojiandaa kuhudumu kwa muhula wa pili madarakani na kumhakikishia ushirikiano wa Kenya na kwa utawala wake .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here