Rais Assouman wa Comoro anavyoizungumzia amani ya Tanzania

0
Rais wa Visiwa vya Comoro, Azali Assouman na mkewe wakiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere(JNIA), kwa kutumia Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania), baada ya kushuhudia Hafla ya Uapisho wa Rais Magufuli iliyofanyika Novemba 5, 2020 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma na Baadaye walitembelea Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro

NA MWANDISHI MAALUM

Amani ni suala muhimu kwa Mataifa yote Duniani na ili mataifa na Watu wake waweze kupiga hatua za kimaendeleo ni muhimu kuimarisha Amani ambayo ndio msingi na ustawi wa kijamii na kiuchumi.

Mambo tunayoyashuhudia kwenye nchi zilizopoteza Amani ni ya kusikitisha na sisi kama nchi ya Tanzania tunapaswa kuziombea Amani nchi hizo ambazo nyingi wakazi wake wanaishia kuwa na maisha magumu na wengine kuishia kuzikimbia nchi zao.

Takwimu za mwaka 2019 na 2020 zilionesha Tanzania imeongoza Afrika Mashariki kwa mujibu wa ripoti ya Global Peace Index (GPI) inayotolewa na taasisi ya uchumi na amani (IEP)yenye makao yake makuu mjini Sydney nchini Australia.

Tanzania ilishika nafasi ya 7 kwa kuwa nchi yenye amani kwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara na duniani ikiwa imeshuka kutoka nafasi ya 51 mwaka 2018 hadi nafasi ya 54 mwaka 2019 kati ya nchi 163, huku Iceland, New Zealand, Uholanzi, Austria, Denmark, Canada, Singapore, Slovenia, Japan, na Jamuhuri ya Czech ni nchi zilizoorodheshwa kuwa na amani zaidi duniani.

Wakati Tanzania ikiongoza Afrika Mashariki, Rwanda imeifuata ikiwa ya pili Afrika Mashariki lakini imeshika nafasi ya 17 kwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara, ikifuatiwa na Uganda iliyoshika nafasi ya 23 , Kenya ya nne Afrika Mashariki na 28 katika nchi za
kusini mwa jangwa la Sahara.

Tanzania tumebarikiwa kuwa na Amani ambayo tangu kuasisiwa kwa nchi yetu Amani imekuwa ni jambo la kipaumbele kwa viongozi wetu wote wakuu wan chi pamoja na watanzania kwa ujumla.

Jambo la kujivunia kwa watanzania ni kwamba Amani na mshikamano umekuwa ni wa kiwango cha hali ya juu na hata mataifa mengine yanatamani, Watanzania ni wamoja, na ukitembelea mahali popote pale watanzania wanafurahia matunda ya Amani na umoja wa
nchi yao yaliyoasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume ambayo mpakasasa yameendelea kuenziwa na Rais Dk. John Magufuli.

Watanzania ni watu wa makabila, Dini, Rangi na itikadi za kisiasatofauti lakini siku zote watanzania ni wamoja na hakuna suala laubaguzi wa aina yoyote ile.

Uchaguzi umemalizika na katika mchakato mzima wa uchaguzi kulikuwa na watu wenye itikadi mbalimbali za kisiasa, kulikuwa na kupigiana kampeni katika uchaguzi huo, na kampeni zilienda kwaAmani na usalama huku kila raia wa nchi hii akiheshimu mawazo na
itikadi ya mwenzake.

Vyombo vya ulinzi na usalama vilisimama katika kuhakikisha kunakuwa na hali ya usalama na mambo yalienda shwari kabisa suala ambalo limeyafanya mataifa mbalimbali kuiona Tanzania ni mfano wa kuigwa.

Rais wa Visiwa vya Comoro, Azali Assouman yeye kwa upande wake amesema Tanzania ni mfano wa kuigwa katika kuimarisha Amani Duniani kutokana na kile alichikushuhudia katika mchakato mzima wa uchaguzi mpaka kufikia tamati yake Oktoba 28 na baadae uapisho wa Rais Dk. John Magufuli Novemba 5 mwaka huu.

Azali amesema alichokishuhudia ni kwamba mchakato mzima ulikuwa huru na haki na alichopendezewa Zaidi ni kuungana kwa wagombea wa urais wa vyama vya upinzani kumpongeza Rais Dk. John Magufuli suala ambalo ni mara chache kutokea kwenye
mataifa mengi Duniani.

“Nilikuja Tanzania kwenye uapisho wa Rais Magufuli, nilichokishuhudia ni cha kupongezwa, mchakato ulikuwa mzuri na natumaini Wabunge wote waliochaguliwa wataendeleza Sera ya Rais Magufuli ya kuiletea Tanzania maendeleo” alisema Rais Assouman.

Rais Assouman katika siku saba alizokuwepo nchini Tanzania alifanya Utalii ambapo alitembelea hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ili kujionea mandhari nzuri ya hali ya hewa ambapo anawataka walii Duniani kutembelea vivutio hivyo.

“Nilipokuwa hapa Tanzania nilipata fursa ya kutembelea hifadhi ya Ngorongoro, hii ni hifadhi ya kipekee kabisa, sasa naondoka kurudi Comoro lakini naomba tu niseme kuwa Tanzania ni nchi nzuri kwa utalii pia nawaomba watalii waje kuangalia vivutio hivi” alisema Rais Assouman.

Rais Azali Assouman wa Comoro aliwasili nchini kwa ajili ya kushuhudia uapisho wa Rais Magufuli uliofanyika Novemba 5 mwaka huu ambapo akiwa nchini alitembelea hifadhi ya Ngorongoro na alirejea nchini kwake Novemba 10 mara baada ya kukaa nchini kwa muda wa siku saba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here