Raia wa Misri wapiga kura duru ya pili

0

CAIRO, MISRI

RAIA wa Misri wanapiga kura katika duru ya pili na ya mwisho ya uchaguzi wa bunge. Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa tatu asubuhi katika majimbo 13 kati ya majimbo 27 ya Misri, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Cairo na sehemu ya kaskazini ya Rasi ya Sinai.

Kulingana na taarifa za ikulu, Rais Abdel-Fatah El-Sissi alipiga kura yake mapema Jumatano. Zaidi ya watu milioni 31 wana haki ya kupiga kura katika duru hiyo ya pili.

Ingawa idadi ndogo ya watu ilijitokeza kupiga kura katika duru ya kwanza, hali iliyoiabisha serikali ya rais el-Sissi. Wakosoaji wanasema bunge jipya halitokuwa na tofauti na lilopita.

Upande wa el-Sissi unatarajiwa kushinda kwa wingi kwenye bunge hilo lenye viti 596.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here