PROF. LIPUMBA AMTEUA MBAROUK SALIM KUWA KAIMU NAIBU KATIBU MKUU CUF ZANZIBAR

0

Mwenyekiti wa CUF- Chama Cha Wananchi Prof. Ibrahim H. Lipumba , kwa kutumia Mamlaka yake ya Kikatiba, amemteua Mheshimiwa Mbarouk Seif Salim kuwa Kaimu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar kuanzia leo Desemba 2, 2020 kupitia barua yenye kumbukumbu Na. CUF/AK/DSM/MKT/07/2020.

Mheshimiwa Mbarouk Seif Salim anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mheshimiwa Ali Makame Issa ambaye Uteuzi wake ulitenguliwa Novemba 8, 2020 kutokana na kwenda kinyume na Msimamo wa Chama.

Kabla ya Uteuzi huu Mheshimiwa Mbarouk Seif Salim alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma.

CUF- Chama Cha Wananchi kinampongeza Mhe. Mbarouk Seif Salim kwa Uteuzi huu na kinamtakia Utekelezaji mwema wa Majukumu yake kama Kaimu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here