Prof. Kitila ashinda ubunge Ubungo

0

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la ubungo, Beatrice Dominic amemtangaza Profesa Kitila Mkumbo wa CCM kuwa mshindi katika jimbo hilo.

Beatrice amesema idadi ya ya wapiga Kura waliojiandikisha ilikuwa 349,057 na waliojitokeza kupiga kura ni 89,656 ambapo kura halali ni 88,274 na zilizoharibika ni 1,382.

Msimamizi huyo amesema Profesa Mkumbo amepata kura 63,221 akifwatiwa na mgombea wa chadema Boniphace Jacob aliyepata kura 20,620 huku mgombea wa ACT Wazalendo Renatus Pamba akipata kura 2,188

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here