Prof. Kitila aitaka TIC ijitangaze zaidi

0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uwekezaji) Prof. Kitila Mkumbo (kulia) akipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) alipofanya ziara ya kikazi kituoni hapo jana na kufanyanya mazungumzo na wafanyakazi na menejimenti kuhusu mwelekeo wa sekta ya uwekezaji Tanzania

Na Bethsheba Wambura

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amehimiza Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kujitanua zaidi ili wajulikane kimataifa na  kutangaza fursa za uwekezaji  ilizopo Tanzania kwa wawekezaji wakubwa kwa kupitia majarida na vyombo vya Kimataifa.

Aidha pia Prof. Mkumbo aliitaka TIC kujitangaza ndani ya nchi ili wajulikane majukumu yao kwa wananchi wajue lakini pia watoe elimu ili ijulikane uwekezaji unahitaji nini ili mtu  aweze kuwekeza.

Prof. Mkumbo aliyasema hayo jana alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za TIC zilizopo  jijini Dar es Salaam na kuzungumza na wafanyakazi na menejimenti ya kituo hicho kuhusu mwelekeo wa sekta ya uwekezaji Tanzania.

Akizungumza na wanahabari baada ya mkutano mkumbo alisema “Kitu kikubwa hapa ni kwamba yapo mambo mawili ya msingi tumezungumza, moja ni kutekeleza lile agizo la Rais kwamba muwekezaji akifika hapa mambo yake yote na taratibu za uwekezaji zikamilike ndani ya siku 14, nilikuwa napitia mifumo kujiridhisha kwamba jambo hilo linawezekana na nimefurahi hukuona kwamba linawezekana.

“Pili, nimetoa hamasa kwa wenzangu hawa wa TIC waweze kujitanua zaidi ili wajulikane majukumu yao kwanza ndani ya nchi ili wananchi wajue majukumu yao na kjuwaoa elimu juu ya uwekezaji.

“Nje wajitangaze na hasa kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania kwa wawekezaji wakubwa kwa kupitia majarida na vyombo vya Kimataifa, mfano wa majarida hayo ni New African, hili ni jarida kubwa kabisa linalozunguzmia masuala yote ya uwekezaji Afrika lakini pia kuna African Business na Foreign Affairs,haya ndiyo majarida ambayo wababe wa uchumi duniani wanayasoma, tukijifungia tu hapa ndani na vyombo vyetu vya habari hatuwezi kujulikana,” alisema.

Waziri huyo pia alisema amewapa TIC  baadhi ya malengo ya Serikali ili kuona kwamba katika muda wa miaka mitano mambo gani yafanyike katika sekta ya uwekezaji.

“‘Kituo chetu cha uwekezaji ndicho kimepewa mamlaka kisheria kusimamia, kuvutia na kutengeneza mazingira ya uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani na nje, nikiwa kama Waziri wa uwekezaji ilikuwa muhimu nifike hapa Ili kujifunza shughuli zao lakini pia kuwapa mwelekeo wa Serikali kuhusu uwekezaji kwa miaka mitano

“Nimezungumza nao ili kubadilisha mifumo yao ya utendaji na mitazamo yao ili kuona nchi yetu inatuvutia wawekezaji kutoka nje na pia wawekezaji wa ndani wanahamasishwa kuchukua nafasi yao kwasababu uchumi wetu unapoelekea unakuwa na hakuna shaka njia mpya ya kukuza uchumi lazima uwekezaji uhusike,” alisema Prof. Mkumbo.

Katika hatua hatua nyingine aliiagiza TIC kutoa ripoti kila baada ya miezi mitatu ya maendeleo ya uwekezaji nchini  ili kujua kwamba wamevutia wawekezaji gani wa ndani na nje katika maeneo yapi, wameleta mtaji kiasi gani, ajira kiasi gani zinazalishwa na zinakwenda kuzalishwa.

Aidha aliitaka TIC kuimarisha uhusiano na ushiriki na taasis  zingine za serikali zinazojihusisha na uwekezaji ikiwamo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Tuje ne uwezo wa kufanya uchambuzi kama njia ya kuwashawishi wenzetu, nimekemea tabia ya kulaumina kwamba anayekwisha hapa ni TRA au NEMC (Baraza la Taifa la Mazingira), nadhani kila mtu ana nia njema na nchi yetu muhimu kwamba kila mtu asaidiwe kutimiza malengo yake katika eneo lake, tukiyafanha haya nchi yetu itakuwa na uwekezaji mkubwa na uchumi utapaaa kwa kasi zaidi, alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here