Polisi Tanzania kuwachezesha Simba SC ‘Mpira mchakamchaka’ leo

0

NA KELVIN SHOO, TUDARCO

TIMU ya Polisi Tanzania imewatahadharisha Simba SC kuwa wastarjie kupata mteremko katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Slaam leo.

Ikumbukwe Simba SC, wanarejea katika ligi kuu baada ya kukamilisha majukumu ya michezo ya Klabu Bingwa Afrika ambapo walifanikiwa kusonga mbele katika raundi ya pili kwa kuwakabili Platnum ya Zimbabwe hivi karibuni.

Akizungumzia mchezo huo, Msemaji wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro, alisema mchezo huo utakuwa mgumu kinyume na baadhi ya mashabiki wanavyofikiri.

Lukwaro alisema kuelekea mchezo huo maandalizi yalikwenda vizuri chini ya Kocha Mkuu, Malale Hamsini lakini pia viongozi wengine kushikamana ili kuhakikisha wanaondoka na alama tatu kwa Mkapa leo.

“Tunakwenda kwa slogani yetu kwamba Umoja wetu ndio nguvu yetu lakini pia tunaongezea na kingine kidogo kwamba tutakuwa na Mpira Mchakamchaka, mtu anakimbizwa mpaka ulimi unamtoka nje,”alisema Lukwaro.

Lukwaro, alisema licha ya Simba kupata ushindi wa michezo yote miwili msimu uliopita lakini wanaamini kuwa leo watatoa ushindani wa hali ya juu kwa hiyo hautakuwa mchezo rahisi kwao.

“Kwa hiyo niseme kwa kesho (leo), mpira utaonekana, burudani pia itaonekana kuhakikisha kwamba Polisi Tanzania tunaibuka na ushindi wa alama tatu muhimu,”alsema Lukwaro.

“Nikweli, niseme kwamba mchezo huo, tunatarajia utakuwa mgumu kwa sababu tunacheza na timu ambayo ni wa wakilishi wa kwetu katika michuano ile ya CAF.

“Kwa hiyo tunajua tunakwenda kucheza na timu kongongwe, tunawaheshimu lakini hatutawaogopa kama ilivyo desturi yetu sisi huwa hatuogoi na hatujawahi kushindwa,”alisema Lukwaro.

Hata hivyo, Lukwaro aliwahakikishia mashabiki wao kwamba kutokana na maandalizi waliyofanya leo wanakwenda kufanya vizuri katika mchezo huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here