Polisi Nigeria yaagiza uhamasishaji baada ya ghasia

0

LAGOS, NIGERIA

INSPEKTA Jenarali wa Polisi nchini Nigeria M.A Adamu, ameagiza uhamasishaji wa haraka wa maafisa wote wa polisi ili ‘kurudisha nafasi ya umma kutoka kwa wahalifu wanaojisingizia kuwa waandamanaji’.

Hatua hiyo inakuja baada ya siku za kadhaa za maandamano ya amani dhidi ya dhuluma za polisi na kisha machafuko ya vurugu ambayo yalisababisha vifo vya takriban watu 69 hadi sasa.

Agizo hilo la polisi huenda likachochea kuongezeka kwa hali ya wasiwasi nchini humo katika ghasia mbaya zaidi kuwahi kutokea katika muda wa miaka kadhaa.

Katika taarifa, Adamu aliwaagiza maafisa wenzake wa polisi kudhibiti nafasi ya umma akisema ghasia zilizoko zimetosha.

Siku ya wiki iliyopita, raia wa Nigeria walitazama kwa hofu wakati wanajeshi walipofyatua risasi dhidi ya waandamanaji wa amani wengi wao wakiwa vijana waliokuwa wakiimba wimbo wa taifa jijini Lagos, huku ripoti ya shirika la Amnesty International ikisema kuwa angalau watu 12 waliuawa.

Matukio nchini Nigeria yamefananishwa na vuguvugu la ”maisha ya watu weusi ni muhimu” nchini Marekani na ufyatuaji risasi wa wanajeshi umeibua shtuma za kimataifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here