Polisi Dar yaua jambazi, yakamata silaha mbili zenye risasi tisa

0
SACP Camillius Wambura,

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limefanikiwa kumuua jambazi mmoja na kukamata silaha mbili aina ya Mark IV na Bastola aina ya Revolver ambayo ilikuwa na risasi 9 ndani ya magazine.

Taarifa hiyo imetolewa leo Desemba 10, 2020, na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Camillius Wambura, na kusema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Desemba 10, 2020, maeneo ya Kimara Korogwe.

“Jambazi huyo aliyekuwa na wenzake wawili waliofanikiwa kukimbia wamekuwa wakijihusisha na matukio ya uhalifu katika Jiji la Dar es Salaam na mikoa Jirani, ambapo mnamo Desemba 7, 2020, majira ya saa 4:00 usiku huko maeneo ya Tabata Msimbazi walipora fedha kiasi cha Tsh 7,800,000/= na simu saba za aina mbalimbali katika duka la wakala wa huduma za kibenki na wakala wa mitandao ya simu”, amesema SACP Wambura.

Aidha SACP Wambura, amesema kuwa majambazi hao walifanya tukio lingine huko Kimara, siku ya Novemba 13, 2020, majira ya saa 3:00 usiku, maeneo ya Mbezi Luis, majambazi hao wapatao wanne wakiwa na silaha aina ya Bastola na Mark IV walipora kiasi cha Tsh 20,000,000/= katika duka la wakala wa benki, mitandao ya simu na bidhaa mbalimbali.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mlonganzila.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here