Pochettino achekelea kupata kazi PSG

0

PARIS, UFARANSA

ALIYEKUWA kocha wa zamani wa Klabu ya Tottenham, Southampton na Espanyol, Mauricio Pochettino, amesaini dili la mwaka mmoja kuinoa Klabu ya PSG.

Mkataba wake ambao unameguka Juni 2022 una kipengele cha kuongeza mwaka mwingine wa ziada ikiwa mabosi wa timu hiyo watapendezwa na mwendo wake na kama itakuwa tofauti atafungashiwa mabegi yake.

Pochetino ambaye aliwahi kucheza ndani ya kikosi hicho msimu wa 2001-2003 anachukua mikoba  ya Thomas Tuchel ambaye alifutwa kazi ndani ya kikosi hicho kutokana na mwendo mbovu wa matajiri hao ambao wanahitaji kubeba makombe mengi.

Baada ya kusaini dili hilo kocha huyo ambaye hakuwa na kazi baada ya kufutwa ndani ya kikosi cha Tottenham Novemba 2019 amesema kuwa anafuraha kubwa kuwa ndani ya kikosi hicho na anaamini kwamba kila kitu kitakwenda sawa.

“Nina furaha ya kweli na ninajivunia kuwa kocha mpya ndani ya Paris Saint-Germain, nimerudi ndani ya timu nikiwa na mipango, hesabu na mbinu mpya,”alisema Pochettino.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here