Petr Cech arejea Chelsea kwa dharula

0

LONDON, UINGEREZA

KIPA wa zamani wa Arsenal na Chelsea,  Petr Cech amerejea tena kwenye timu yake ya zamani ya Chelsea akiwa ni mshauri kwenye masuala ya ufundi kwa makipa.

Pia jina la nyota huyo limeorodheshwa kwa makipa ikitokea dharula anaweza kuanza kikosi cha kwanza ndani ya Ligi Kuu England pamoja na mashindano mengine.

Kipa huyo mwenye miaka 34 ameteuliwa na Kocha Mkuu wa Chelsea, Frank Lampard ambaye amevutiwa na rekodi zake zama hizo alipokuwa ndani ya uwanja.
Kiongozi wa Chelsea inayotumia Uwanja wa Stamford Bridge, Marina Granovskaia amesema kuwa wamefurahi kuona Petr amerejea nyumbani.

“Tuna amini katika kufikia mafaniko ambayo tunahitaji, kwa kuwa amerejea nyumbani basi kazi itakuwa moja kupata kile ambacho anacho kwa manufaa ya timu kiujumla,”alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here