Patrick Rweyemamu afutwa kazi Simba SC

0

NA MWANDISHI WETU

IMEELEZWA kuwa Klabu ya Simba imewafuta kazi Mwarami Mohamed (Kocha wa magoli kipa) na Patrick Rweyemamu (Meneja wa timu ) kutokana na matokeo mabaya kwa mechi mbili  Mfululizo 

Simba imecheza mechi mbili mfululizo na kupoteza pointi sita ambapo ilianza kufungwa bao 1-0 mbele ya Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela na ikachapwa tena bao 1-0 mbele ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Uhuru.

Kwenye mechi mbili ambazo zilikuwa zinahusisha timu za majeshi wenye mwendo wa kucheza ligwaride, Simba imeyeyusha pointi sita na kufungwa mabao mawili.

Pia inaelezwa kuwa wangine ambao wamefutwa kazi ni Ally Shatry ‘Bob Chico’ na  Jacob ambao  walikuwa kwenye  kitengo cha Habari cha Klabu hiyo.

Wawili hao wamefutwa kazi  kwa kile kinachosadikika kuwa karibu na CEO wa zamani Senzo Mazingiza ambae hivi sasa yupo Yanga.

Patrick Rweyemamu ambaye anatajwa kufutwa kazi hakuwa tayari kuzungumzia hilo pamoja na Katibu Mkuu wa Simba, Arnold Kasehembe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here