‘Pacha’ wa Harmonize aibuka Mbagala

0

NA IRENE SABAS , TUDARCO

MSANII Followzee kutoka Mbagala jijini Dar es Salaam, amesema anasikia raha sana watu kumfananisha na kuitwa pacha wa Harmonize kwani msanii huyo ni mmoja wa wasanii wakubwa kwa sasa Tanzania.

Followzee, alisema yeye ni mwanafamilia wa lebo ya Konde Gang ambayo anaimiliki Harmonize japo hawaishi pamoja wala hawana undugu, ila ni mwanafamilia kwa sababu wanashea kabila moja la Kimakonde na wanatokea Mkoa mmoja wa Mtwara.

“Mimi sio chawa wala mdananda wa Harmonize, huu ndiyo mtindo wangu wa nywele siyo kama namuiga, kuna muda huwa nasuka pia nazipaka rangi.

“Sijiiti bali mashabiki wananiita pacha wa Harmonize na nafananishwa naye, wengi wananiita Konde Boy Jeshi au Tembo na ndiyo majina ambayo anayotumia Harmonize mwenyewe.

“Kwangu ni furaha kufananishwa na Harmonize naona ni kitu kikubwa, sidhani kama anajua kama nafananishwa naye ila naamini ananijua kwani tumeshaonana sehemu nyingi ila hatujawahi kukaa na kuongea,”alisema Followzee

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here