Olenasha ala kiapo cha utii Bunge la Afrika Mashariki

0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, William Tate Olenasha akiapa kiapo cha utii na uadilifu mbele ya Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ngoga Martin

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, William Tate Olenasha, ameapa kiapo cha Utii cha Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Olenasha ameapa kiapo hicho na kushuhudiwa na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Martin Ngoga pamoja na wabunge wengine wanaounda Bunge hilo ili kumwezesha kushiriki kwenye Bunge hilo kama Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Naibu Waziri huyo ameapa kiapo hicho akiwa katika Ofisi za Wizara zilizopo kwenye Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma wakati wa kikao kilichofanyika kwa njia ya mtandao jana Desemba 10, 2020.

Aidha, kikao hicho kilihudhuriwa na Wabunge wa Bunge hilo ambao wengi walishiriki kutokea kwenye nchi zao wakati Spika akiwa Makao Makuu ya Bunge hilo jijini Arusha.

Kikao hicho, pamoja na mambo mengine kimejadili Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Afrika Mashariki ya Masuala Mtambuka.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, William Tate Olenasha akiapa kiapo cha utii na uadilifu mbele ya Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki,Ngoga Martin. kulia ni mbunge wa bunge hilo kutokea Tanzania, Josephine Sebastian Lemoyan

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here