Ole Sendeka ashinda ubunge Simanjiro

0

Mwandishi Wetu

Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Simanjiro, Yefred Myenzi amemtangaza mgombea ubunge wa CCM jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka kuwa mshindi baada ya kupata kura 54,609.

Myenzi amesema mgombea ubunge kupitia Chadema, Emmanuel Landey amepata kura 8,782.

Amesema kwenye jimbo hilo wananchi 133,086 walijiandikisha kupiga kura.

Amesema kati yao waliopiga kura ni 64,238 ila kura halali ni 63,391 na zilizokataliwa ni 847.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here