Nyota walioweka rekodi usajili VPL 2020

0

NA MWANDISHI WETU

SOKA la bongo miaka ya sasa limekuwa tofauti kabisa na miaka ya nyuma. Tofauti na zamani ambapo ukizungumza kuhusu mpira unazungumzia burudani na ushabiki, na umaarufu wa wachezaji, sasa hivi ukizungumza mpira unazungumza pesa.

Hivi sasa hakuna mchezaji anayecheza au kufikiria kucheza mpira kwa lengo la kupata umaarufu. Kila mtu sasa hivi kwenye mpira wa soka anafikiria aende klabu kubwa apate pesa. Na wapo baadhi ya mastaa ambao wamevunja rekodi kwa kuvuta pesa nyingi katika sajili zao lakini posho ambazo wanaendelea kuchukua kutokana timu zao kuibuka na matokeo mazuri katika michezo mbalimbali ya Ligi Kuu Bara pamoja na michuano mingine.

BAKARI MWAMNYETO

Beki wa kati wa Yanga usajili wake ulikuwa wa vuta nikuvute kutokana na kuhitajika na timu tatu kubwa hapa nchini Simba na Azam ambao walishindwa kumpata kutokana na pesa ambayo ilikuwa inahitajika na mchezaji mwenyewe pamoja na timu yake ya Coastal Union ya Tanga.

Baada ya ushindani huo wa vigogo Yanga walifikia makubaliano na mchezaji huyo kutoa Sh milioni 150 ili kumpata Mwamnyeto ambaye kuna pesa yake alichukua ambayo haikuwa chini ya Sh milioni 70 na nyingine iliyobaki ilikwenda Coastal Union kutokana alikuwa bado na mkataba wa mwaka mmoja pamoja na wasimamizi wake.

TUISILA / MUKOKO

Wakongomani wawili wa Yanga, Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe walisajiliwa na kikosi hiko kutokea AS Vita inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini kwao.

Nyota hao wawili waliosajiliwa katika dirisha kubwa la usajili kwa kuwa walitoka katika kikosi kimoja usajili wao ulikuwa Dola za Kimarekani 130,000 ambayo kwa pesa ya kibongo inakuwa zaidi ya Sh milioni 300. Ukiachana na pesa hiyo ya usajili ambayo ni mkwanja mrefu ambao nyota hao walivuta wamekuwa wakichukua posho mara kwa mara kutokana na matokeo ambayo wamekuwa wakiyapata katika kikosi cha Yanga msimu huu.

Yanga kabla ya msimu kuanza uliweka hadharani watakuwa wakitoa posho kwa wachezaji wao kama watashinda michezo mitatu mfululizo huku wachezaji ambao watacheza watakuwa wanapata nyingi kuliko wale ambao watakuwa nje.

BERNARD MORRISON

Winga huyu wa Simba alisajiliwa kwa mbwembwe na alitikisa katika vyombo vya habari, vijiwe vya soka na maeneo mengine mbalimbali akitokea Yanga na gharama yake ya usajili ilikuwa ni Dola za Kimarekani 85,000 ambazo kwa pesa ya Kitanzania inakuwa zaidi ya Sh milioni 196.

Baada ya kuvuta mkwanja huo mrefu wa usajili tena kimya kimya alionekana kucheza katika kikosi cha Simba mwanzo wa msimu kama moja ya wachezaji aliyekuwa akiwafurahisha mashabiki wa kikosi hiko kutokana na mambo ambayo alikuwa akiyafanya.

Miongoni mwa raha ambazo Morrison alikuwa akiwapa mashabiki na wapenzi wa Simba ni mabao mawili ambayo alifunga dhidi ya Vital’O ya Burundi na Namungo katika mechi ya ufunguzi wa msimu huku akisababisha penati ambayo John Bocco alikwenda kufunga kwa penalti.

Mabosi wa Simba huwa na utamaduni wa kutoa posho Sh 300,000 kwa kila mchezaji ambaye amecheza katika mchezo wa ligi ambao wameshinda, 200,000 kwa wale ambao watakuwa benchi lakini hawakuingia, Sh 100,000 kwa wale ambao hawakuwepo hata katika benchi la akiba.

PRINCE DUBE

Ana mabao sita na ndio kinara wa mabao katika kikosi cha Azam, usajili wake wala haukuwa na maneno mengi au kufatiliwa na mashabiki wengi wa soka hapa nchini lakini moto wake aliokuwa akionyesha uwanjani kabla ya kuumia ni jambo ambalo lilikuwa likifuatilia na wapenzi wengi wa soka. Kitita cha pesa ambacho amevuta kutoka katika kikosi hiko katika usajili wake si chini ya Sh milioni 70.

RALLY BWALYA

Yanga walikuwa tayari wameshaanza mazungumzo na wakiamini kabla ya msimu huu kuanza watakuwa wamemsajili kiungo huyo kutokea Power Dynamos inayoshiriki Ligi Kuu ya Zambia lakini kilicho watokeo wapinzani wao Simba wakamalizana na nyota huyo juu kwa juu.

Simba walimsajili Bwalya kwa mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Dola za Kimarekani 50,000 ambayo kwa pesa ya hapa nyumbani ni zaidi ya Sh milioni 100. Bwalya aliyeanza kuonyesha makali yake katika tamasha la Simba (Simba Day), akipiga pasi tamu ya mwisho iliyokwenda kuzaa bao la Morrison ni moja ya wachezaji ambao wamevuta mkwanja mrefu katika usajili wa dirisha kubwa.

CHRIS MUGALU  

Kutokana bado alikuwa na mkataba na timu yake ya Lusaka Dynamos ambayo inashiriki Ligi Kuu ya nchini Zambia lakini maelewano mazuri ya viongozi wa juu, Simba walitakiwa kulipa Dola 70 zaidi ya Sh milioni 140 kwa pesa ya Kitanzania ili kunasa saini ya straika huyo.

Kutokana na Simba walikuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu wala hawakutaka kulaza damu walitoa kiasi hiko cha pesa na walikamilisha dili la Mkongomani huyo ambaye anauwezo mkubwa wa kucheza na nyavu katika nafasi chache za kufunga ambazo anapata pindi anapokuwa uwanjani

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here