Nkamia achukua fomu ya kugombea uenyekiti Simba SC

0

NA MUSSA KICHEBA

ALIYEKUA Mbunge wa Jimbo la Nchemba (Awali lilifahamika kama Kondoa Kusini), Juma Nkamia ni miongoni mwa wanachama wa klabu ya Simba SC waliojitosa kuchukua fomu za kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa ndani wa klabu hiyo.

Simba SC, ipo kwenye mchakato wa  kuziba nafasi ya mwenyekiti ambayo kwa sasa inayokaimiwa na Mwina Kaduguda ambapo uchaguzi unafatarajiwa kufanyika Februari 07, mwakani (2021).

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba, Boniface Lihamwike, alisema Nkamia ni sehemu ya wanachama waliojitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo, ili kuziba nafasi ya Swedi Mkwabi aliyejiuzulu mwezi Septemba, mwaka jana.

Lihamwike pia akawataja waliochukua fomu za kuwani nafasi hiyo mpaka sasa ni Hassan Dalali, Ayubu Semvua, Victor Antony, Mohamed Soloka, Kassim Nyangalika, Rashid Shangazi na Piton Mwakisu.

Wengine ni Hamisi Omary, Mutaza Mangungu pamoja na mwanahabari mkongwe na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Nchemba lakini na Simba wa kulialia, Juma Nkamia.

Katika hatau nyingine kiongozi huyo aliongeza kuwa, kamati yake inaendelea na zoezi la utoaji wa fomu za kugombea kwa wanachama ambalo siku hadi siku linaendelea kuchanganya kutoka na wengi wao kupata muitikio wa kutosha kutoa kwenye vyombo vya habari.

 “Tunaendelea na zoezi letu la uchukuaji fomu ambalo awali lilianza kwa kulega kutokana na wajumbe kutojitokeza.”

“Tunaamini hadi siku ya mwisho watu wengi zaidi watajitokeza kuchukua fomu ili kutimiza matakwa ya kikatiba ndani ya Simba. Nimekuwa nikipokea simu nyingi sana kutoka kwa wajumbe mbalimbali kuhitaji kuchukua fomu,”alisema Lihamwike.

Zoezi la uchukuaji fomu linatarajiwa kufungwa kesho Desemba 24 ambapo lilianza Desemba 14.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here