Nini hasa chanzo cha mzozo unaendelea kaskazini mwa Msumbiji?

0

NA MWANDISHI WETU

Idadi ya raia waliolazimishwa kuyakimbia makazi yao kutoka na mzozo katika eneo la Kaskazini mwa Mshumbiji imeongezeka mara nne mwaka huu na kufikia hadi watu 420,000 – kulingana Umoja wa Mataifa.

Unuhusisha mzozo katika jimbo la Cabo Delgado si kwa mashambulio ya wapiganaji wa kiislamu tu, lakini pia na kuhindwa kugawanywa kwa mapato makubwa ya madini na gesi miongoni mwa wakazi wa eneo hilo.

Afisa wa ngazi ya juu wa Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa anayelitembelea jimbo la Cabo Delgado alielezea hali katika jimbo hilo kama “mbaya sana na ya darura ” na akazitaka nchi jirani na Msumbiji na jamii ya kimataifa kwa ujumla kuingilia kati kile alichokieleza kuwa umekuwa mzozo wa muda mrefu “usioonekana”.

“Idadi inaongezeka kadri muda unavyokwenda na hii ni hali ambayo inaweza kuwa mbaya zaidi ,” amesema Angèle Dikongué-Atangana,naibu mkurugenzi wa UNHCR kanda ya Afrika Ksuini, alipozungumza na BBC kutoka jimbo la Cabo Delgado, Pemba.

Dikongué-Atangana ameonya kuwa hali ya “ugaidi ” nchini Msumbiji imeanza kufanana na mzozo wa muda mrefu wa kaskazini mwa Nigeria, ambako kikundi cha wanamgambo wa kiislamu cha Boko Haram kimesababisha madhara makubwa.

Lakini pamoja na kuwalaumu wanamgambo wenye uhusiano na Kikundi cha Islamic State waliotekeleza mauaji ya kikatili na maafa mengine katika jimbo la Cabo Delgado, Bi Dikongué-Atangana amekosoa tabia ya “makampuni ”uchimbaji ” yanayohusika na uchimbaji wa madini na uchimbaji wa gesi kwenye fukwe ‘Bila matumaini , hakuna ndoto ‘

“Kama nilizaliwa katika eneo kama hili, ambalo lina utajiri mkubwa , na ninaona utajiri unaporwa, na sioni…sehemu ya utajiri, pia hata mimi ningekasirika ,” alisema, akionya kuwa kizazi cha vijana cha Mshumbiji ambacho “hakina matumaini , wala hakina ndoto ,” kinaweza kujiunga na makundi yanayovuruga usalama : “Kama ninapigana , labda ninaweza kufa kwa kifo cha heshima . Kama nisipopigana, labda bado ninaweza kufa”.

Katika miezi ya hivi karibuni, bandari ndogo ya Pemba, imekuwa na shughuli nyingi kupita kiasi, idadi ya wakazi wa eneo hilo iliongezeka karibu mara dufu , huku maelfu ya watu wakiwasili kwa miguu au kwa maboti, wakikimbia ,mashambulio yyenye utata na ya kikatili ambayo yamekuwa yakiongezeka bila kikomo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

”Hakuna chochote nilichobakisha, nina hili boti tu ,” mvuvi , Wazir aliliambia shirika la habari la AFP . Mke wake , Aziza Falume, alijifungua ndani ya bahari walipokuwa katika boti lao wakiyakimbia mashambulio.

“Bado ninahofu. Ninajiuliza tu wakati wote ni lini wapiganaji wa Jihadi watakuja Pemba na kushambuli, au kama kuna mmoja wao anayeishi miongoni mwetu ,” alisema.

Wizara ya mambo ya nje ya Marakeni sasa imeonya kuwa Pemba “inaweza kushambuliwa kwasababu iko karibu zaidi na vikosi vya waopiganaji vinavyoendesha mashambulio ya ghasia”

Serikali ya Msumbiji – ambayo hadi sasa imekuwa ikitegemea msaada wa wanajeshi kutoka kwa wajenzi kutoka Urusi na Afrika Kusini- kwa sasa inakabiliwa na shinikizo la kukubali usaidizi mkubwa au uingiaji kati wa majirani zake, ambao wanahofia hali mbaya ya usalam ambayo imeanza kuvuka mipaka.

Lakini mzungumzo yanoanekana kuzorota, huku Msumbiji ikiwa na wasiwasi kuhusu ushawishi wa nje na kuonekana kwa kushindwa kwa serikali hyake kutatua mzozo huo. Wakati huo huo, ukosoaji wa kigeni kwa Msumbiji juu ya namna inavyoshughulikia mzozo huo pia umekuwa mkali.

Waziri wa mahusiano ya kimataifa wa Afrika Kusini Naledi Pandor, alizungumzia “mapungufu ya utawala, ukiukaji wa haki za binadamu, na mzozo juu ya raslimali “.

Kundi la baraza la maaskofu wa Afrika Kusini ambao walitembelea mji wa Pemba hivi karibuni lilitoa taarifa iliyosema : ” Karibu kila mtu alizungumzia kukubali kuwa vita vya Mshumbiji ni kuhusu makampuni ya kimataifa yanayopigani kupata udhibiti wa madini ya jimbo na raslimali ya gesi, kwa kupunguza idadi ya watu katika maeneo ya mwambao “.

Na mjini Brussels, Waziri wa Muungano wa Ulaya wa Masuala ya kigeni Josep Borrell Fontelles pia alitoa tathmini yake kali kuhusumapungufu ya Msumbiji : “Hatuwezi kusema kwamba kila kitu kinatoake Msumbiji kinasababishwa na sehemu ya vuguvugu linaloitwa Wanamgambo wa Kiislamu.

“Kwa kiasi fulani hilo ni kweli. Lakini ghasia za silaha katika eneo la kaskazini mwa Msumbiji zilichochewa na umasikini na ukosefu wa usawa miongoni mwa wakazi wa eneo waliokosa heshima kwa taifa ambalo halikuweza kuwapatia walichohitaji ,” aliongeza.

“Msumbiji ina hifadhi ya tatu kwa ukubwa ya gesi barani Afrika baada ya Nigeria na Algeria . Unaweza kufikiria kwamba hii inawafanya raia wahisi wametengwa .Ni nchi tajiri na wanaishi kwa umasikini .

Kwa kiasi kikubwa serikali ya Msumbiji imekuwa ikitaka kulaumu kuwa mzozo unachochewa na wapiganaji wa jihadi wa kigeni, zaidi ya kukiri kuwa mzozo huo umesababishwa na uasi ulioibuka ndani ya nchi.

“Magaidi wanawauwa watu na kusababisha kusambaratika. Katika kukabiliana na magaidi serikali imejibu vikali…kwa usaidizi wa watu wa eneo ” alisema Rais Filipe Nyusi, mapema mwaka huu.

Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi

Mkurugenzi wa UNHCR, Dikongué-Atangana amekiri ugumu wa hali katika jimbo la Cabo Delgado, na akasema kwamba huku suala la ufisadi na utawala bora vikiwa muhimu, tisho la kwanza ni ” ugaidi kwa kiasi kikubwa

“Kwahiyo wito wangu halisi ni kwamba jamii ya kimataifa inapaswa kusema ukweli kuanza kuangazia hali inayoendelea hapa Msumbiji.”

CHANZO: BBC

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here