Nigeria: Polisi yaua 12, yajeruhi

0

LAGOS, NIGERIA

Shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty International limedai watu wasiopungua 12 wameuawa na wengine wamejeruhiwa wakati Vikosi vya Serikali vilipowafyatulia risasi waandamanaji eneo la Lekki Mjini Lagos.

Shirika hilo linalotetea Haki za Binadamu limesema uchunguzi umebaini ushahidi wa vifo 12 huku mamia wakijeruhiwa. Pia, wametuhumu Polisi na Wanajeshi kwa kutumia nguvu kupita kiasi.

Pamoja na kutokea kwa vifo hivyo bado makundi makubwa ya waandaamanaji wameendelea kuingia mitaani na kuanza kuchoma matairi moto, huku wakiimba wimbo wa taifa hilo.

Watu maarufu nchini humo akiwemo msanii Davido wameungana na waandamanaji waopinga vikali vitendo hiyo, akitumia mtandao wa Instagram kumwonyesha Rais Mahamoud Buhari na kusema “tulikosea kukuchagua haya ndio malipo yake.”

Hata hivyo, Gavana wa Mji huo, Babajide Sanwo-Olu amethibitisha zaidi ya majeruhi 20, lakini akasema hakuna mtu aliyepoteza maisha.

Watu maarufu duniani wakiwemo Beyonce, Kanye West, Rihanna, Hillary Clinton wamepaza sauti kuhusu maandamano hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here