Nigeria: Mwanasheria ataka maandishi ya kiarabu yatolewe kwenye fedha, nembo ya jeshi

0

LAGOS, Nigeria

Mahakama mjini Lagos Nigeria inatarajia kusikiliza kesi iliyofunguliwa na mwanasheria Malcom Omirhobo dhidi ya Benki Kuu ya Nigeria akitaka kuondolewa kwa maandishi ya kiarabu kwenye fedha za nchi hiyo.

Omirhobo pia anataka jeshi la Nigeria kuondoa maandishi kutoka kwenye nembo ya jeshi yanayoashiria kuwa Nigeria ni nchi ya Kiislamu, kinyume na katiba ya nchi hiyo kuwa ni taifa lisilofungamana na dini yoyote.

Mwanasheria huyo anataka maandishi hayo yawekwe kwa lugha ya Kiingereza au kwa lugha yoyote miongoni mwa lugha tatu zinazotumika nchini humo –Hausa, Yoruba au Igbo. Hatahivyo, Benki Kuu imekana kuwa maandishi hayo ni ishara ya Uislamu.

Watu wengi nchini humo, hasa eneo la Kaskazini, huongea Kiarabu. Hata hivyo Kiingereza ni lugha kuu ya mawasiliano nchini humo.

Nembo ya Jeshi la Nigeria

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here