Nguli wa sheria amlima barua Wakili wa Lissu

0
Wakili Robert Amsterdam

Na MWANDISHI WETU

MWANASHERIA nguli nchini, Alberto Msando, amemwandikia barua wakili wa Mgombea Urais wa Chadema Tundu Lissu, Robert Amsterdams na kumtaka kuacha kuingilia mambo ya Tanzania kwani ni nchi huru.

Msando katika barua hiyo yenye kurasa 11 alielezea upotoshaji mkubwa uliofanywa na Amsterdams kwa kutoa tuhuma zisizo na msingi wala ushahidi dhidi ya Rais Dk John Magufuli na Serikali ya Tanzania.

Msando alisema licha ya Lissu kutamba kuwa amefanya mikutano mingi kuliko Dk. Magufuli lakini wakili wake alidai kuwa kulikuwa na mazingira ya kuvibana vyama vya upinzani visifanye mikutano. Alieleza pia katika mazingira ya Lissu kujaza watu katika mikutano yake lakini wakili huyo alidai kuwa Tanzania hakuna uhuru wa kukusanyika na mikutano.

Msando alimfahamisha Amsterdams kuwa Tanzania ina sheria zake na kwamba hakuna nchi yeyote duniani inayotoa uhuru pasipo kuweka miongozo na taratibu ambazo mtu akizikuka lazima achukuliwe hatua.

Alisema kama Lissu alikiuka taratibu na sheria za nchi lazima awajibike kwani uhuru wa mtu mmoja unaweza kuwa hatari kwa mtu mwingine endapo hautawekewa mipaka.

Msando aliendelea kusema katika barua hiyo kwa wakili Amsterdams ambaye anatuhumiwa kwa kujihusisha na ushoga na kutetea ushoga duniani, kuwa amekuwa akieleza tuhuma za uongo kwa lengo la kuichafua Tanzania na kuonyesha kuwa uchaguzi hauko huru na haki jambo ambalo ni uongo.

Alisema wakili huyo wa Lissu amekuwa akitishia kuwa endapo uchaguzi utakuwa si wa huru na haki basi viongozo waliopo madarakani watashtakiwa katika mahakama za Kimataifa za makosa ya uhalifu.

Hata hivyo Msando alimtaka kueleza ni kosa gani ambalo viongozi wa Tanzania watakuwa wametenda kwa mujibu wa sheria za Kimataifa hadi kusababisha ashtakiwe katika mahakama hiyo ambayo imeanisha aina ya makossa ya mtu kushtakiwa.

Alifafanua kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 17 cha Sheria ya ICC imekubaliwa kuwa sheria yeyote ya Kimataifa lazima ilinde Uhuru wan chi husika na kutokuwepo kwa ushindani baina ya mahakama za ndani na zile za kimataifa. Alisema ni katika mazingira yatakayodhibitisha kuwa mahakama ya ndani haziwezi kumuhukumu katika makosa manne yaliyoainishwa.

Hivyo alimtaka wakili huyo kumtaarifu mteja wake kuwa endapo hataridhika na chochote katika mchakato wa uchaguzi Mahakama za Tanzania zipo huru na ana haki ya kwenda kupinga kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi.

Aidha alimtaka kuiacha Tanzania ifanye uchaguzi kwa amani na kucha kupandikiza vurugu kupitia kwa mteja wake na kwamba Watanzania watailinda amani yao kwa njia zozote na kwa uzalendo mkubwa.

Msando alisema pia jitihada za serikali za kupambana na rushwa, ufisadi na kusimamia rasilimali za watanzania, hazitarudishwa nyuma na mabeberu na vibaraka wao wenye maslahi yao binafsi.

Wakili Alberto Msando

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here