NEC yaongeza siku mbili za kuapisha mawakala wa vyama

0

Na Mwandishi Wetu

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kwa Mamlaka iliyopewa imeongeza muda wa kuwaapisha mawakala wa vyama vya siasa, ambapo zoezi hilo lililoanza leo Oktoba 21, litaendelea hadi Oktoba 23, 2020.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Wilson Mahera amesema ongezeko hilo ni kutokana na uwepo wa changamoto mbalimbali ikiwemo maeneo mengine kutofikika kwa urahisi

Amesema ni lazima vyama vipeleke orodha ya mawakala na kuwapanga katika vituo pamoja na anuani zao na namba za simu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here