NEC yamkabidhi Magufuli cheti cha ushindi

0

Na Dotto Kwilasa, Dodoma 

TUME ya Taifa ya uchaguzi (NEC)imemkabidhi cheti Cha ushindi wa kiti Cha Rais Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 Rais mteule wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli Pamoja na mgombea mwenza mama Samia Suluhu Hassan huku akisema kuwa ana deni kubwa katika kuwatumikia wananchi.
Akizungumza jana mara baada ya kukabidhiwa cheti hicho alisema kuwa uchaguzi wa mwaka huu umefanyika vizuri na kwa kiwango cha juu huku ukijali utu na haki za binadamu.

Mbali na hayo Dk.Magufuli alitumia nafasi hiyo kuwashukuru watanzania kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kumchagua tena kwa ajili ya kuwatumikia katika kipindi kingine Cha miaka 5.

“Mmetupa ushindi ambao umetuachia deni kubwa sana maana kupata asilimia 84.4 ni imani kubwa sana na imani yao nitaitimiza kwa kufanya kazi sana”alisema.

Dk.Magufuli alisema kuwa ushindi huo sio wake bali ni wawananchi wenyewe hivyo atawatumikia wananchi wote bila kujali mahali wanapotoka.

Aidha katika hatua nyingine Rais Magufuli aliipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nakusema kuwa kwa mara ya kwanza kulikuwepo na karatasi maalu kwa watu wasioona.

“Pamoja na hayo lakini pia kulikuwa na vitendea kazi vingi na vyakutosha ndio maana kulikuwa na vituo vingi vya kupigia kura ili kuepusha msongamano”alisema

ATOA SHUKRANI KWA WAGOMBEA WENGINE

Dk.Magufuli aliwashukuru wagombea
wengine waloshiriki katika kinyanganyiro cha kugombea urais huku akiahidi kushirikiana nao katika kuleta maendeleo ya nchi.

“Siasa siyo vita wala siyo vita na katika hilo na katika hilo napenda kuwaahidi kuwa nitashirikiana nanyi kwani maendeleo hayana chama”alisema.

Pamoja na hayo Rais Magufuli amewashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuombea uchaguzi na kuilinda amani.

“Lakini pia navishukuru vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuhakikisha amani inakuwepo tangu kipindi cha mchakato wa uchaguzi mpaka sasa”

PONGEZI KWA CCM

Magufuli amekishukuru chama cha mapinduzi kwa kuweza kumteua tena kuwa mgombea wa urais lakini pia kuwa pamoja naye katika kampeni.

” Ilani ya uchaguzi tuliyokuwa tukiinadi nitahakikisha tunayatimiza yale yote yaliyomo ili kuweza kuleta maendelo katika nchi yetu” alisema.

Hata hivyo Rais Magufuli aliwataka wale wote waliochaguliwa katika ngazi mbalimbali ikiwemo ubunge na udiwani kuwajibika kwa wananchi katika yale waliyoyaahidi.

“Twende tukashikamane kwa pamoja kwa maslahi ya taifa letu kwani maendeleo hayana chama”alisema.

RAIS MSTAAFU WA BURUNDI

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Rais mstaafu wa Burundi Silvester Ntibantunganya ambaye aliwakilisha waangalizi wa uchaguzi mkuu kutoka nchi za Afrika mashariki ambapo alisema uchaguzi ulikuwa huru na demokrasia.

Licha hayo Ntibantunganya alisema mchakato wa uchaguzi nchini hapa unatazamwa na mataifa mengine Kama funzo na kuepusha mtafaruko katika nchi nyingi za kiafrika.

“Dunia imeshuhudia uchaguzi Wenye demokrasia ya hali ya juu na ni matumaini yangu kuwa wengi tumejifunza na kujionea neema iliyopo ya amani na utulivu,”alisema.

Rais Mstaafu wa Burundi, Sylvestre Ntibantunganya

WAWAKILISHI WA VYAMA VINGINE VYA SIASA

Katika hafla hiyo ya utoaji wa cheti kwa mshindi wa kiti Cha Rais ambaye ametokana na Chama Cha mapinduzi (CCM),baadhi ya Wagombea wa kiti hicho ambao kura zao hazikitosha ,Walipata nafasi ya kuzungumza kwa niaba ya wengine huku wakisisitiza kuendelea kishirikiana na serikali bega kwa bega Katika Maendeleo.

Queen Sendiga ambaye alikuwa mgombea wa kiti cha urais kupitia Chama cha ADC mbali na kumpongeza Dk.Magufuli kwa kupata ushindi wa kishindo alimshukuru kwa kuendesha uchaguzi mkuu kwa njia ya demokrasia na amani.

Sendiga alisema,mbali na kwamba kura zake hazikutosha hiyo sio sababu ya yeye kushindwa kishirikiana na Serikali katika kuijenga Tanzania na kuahidi kuendelea kusimama bega kwa bega na Serikali iliyopo madarakani kuwatumikia watanzania.

“Utofauti wa vyama si uadui,nakubaliana kuanza upya kushirikiana kwa vitendo na Viongozi waliopo madarakani Katika kuanza kwa matumaini mapya ya miaka mingine mitano ijayo,”alisema.

Licha ya hayo alimuomba Rais Magufuli kuendelea kuenzi matakwa ya wananchi Katika kuleta maendelo na maisha mazuri hali itakayosaidia zaidi kulinda na kuuheshimu Muungano na amani.

Mbali na hayo Mgombea huyo wa ADC alitumia nafasi hiyo kumuomba Rais Magufuli kutoa ruzuku ya fedha kwa vyama vyote vya siasa nchini ili kuweza kujiendesha.

Aliyekuwa mgombea uraia wa Tanzania kupitia ADC, Queen Sendiga

Kwa upande wa Mgombea wa NRA Leopord Mahona alisema ushindi wa Magufuli ni ishara ya mafanikio ya maendeleo zaidi kwa miaka mingine ijayo.

“Kutokana na ushindi huu tunatarajia mazuri mengi zaidi ,na sisi kama wafuasi wa vyama vingine vya siasa tunaahidi kushirikiana na Serikali ijayo kwa Maendeleo ya watanzania,”alisisitiza .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here