NEC yakanusha uwepo wa masanduku ya kura feki Kawe, Pangani na Buhigwe

0

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kupitia kwa Mwenyekiti wake, Jaji MST. Stemistocles Kaijage amekanusha taarifa zinasombaa mitandaoni juu ya uwepo wa masanduku ya kura feki katika Majimbo ya Kawe (Dar), Pangani (Tanga) na Buhigwe (Kigoma).

Akizungumza na wanahabari katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere kilichopo jijini Dar es Salaam ambapo ndipo shughuli za majumuisho ya matokeo yanakofanyika Jaji Kaijage amesema NEC haijapokea wala kuthibitisha taarifa hizo.

“Tume haijapokea wala kuthibitisha taarifa hizo za uwepo wa masanduku ya kura feki katika majimbo hayo. Niendelee kuwahimiza Watanzania kupuuza taarifa za mitandaoni  ambazo hazijathibitishwa na Tume” amesema Jaji Kaijage na kuongeza;

“Pamoja na uwepo wa changamoto kidogo ikiwamo wapiga kura kukosa majina yao kutokana na kuchelewa kuhakiki taarifa zao Lakini zilitatuliwa na baadae zilitatuliwa. Tume inaendelea kufatilia namna ambavyo Zoezi la uchaguzi linaendelea nchi nzima na itatoa taarifa kwa kadili itakavyowezekana.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here