NEC kuwachukulia hatua wanasiasa watakaoshindwa kuthibitisha madai ya vituo hewa

0

Na Mwandishi Wetu,Dodoma 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma jana Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera amesema tuhuma hizo zinalenga kuzua taharuki kwa jambo ambalo si la kweli.

Akieleza sababu ya vituo vya kupigia kura kuwa vingi kuliko vile vya kujiandikisha kupiga kura, Dkt. Mahera amesema hilo limetokana na kila kituo kuwa na idadi ya wapigakura wasizidi 500 ili kurahisisha zoezi la upigaji kura.

“Vituo vilivyotumika kuandikisha wapiga kura vilikuwa 37,814, na vituo vya kupigia kura ni 80,155, hii inatokana na kwamba kwenye kituo kimoja kilichotumika kujiandikisha kinaweza kutoa vituo vitatu kwa sababu kituo kimoja kinatakiwa kuwa na wapigakura 450 hadi 500.”

Akizungumzi maandalizi ya upigaji kura amesema tayari vifaa vyote muhimu vimefika kwenye majimbo ya Tanzania Bara na Zanzibar, na kwamba zoezi hilo litafanyika kwa ufanisi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here