NEC : Hakuna vituo hewa vya kupigia kura

0

Na Mwandishi Wetu

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchin (NEC) imekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna vituo hewa vya kupigia kura vimeongezwa katika baadhi ya majimbo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 25, 2020 jijini Dodoma Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dk. Wilson Mahera, alisema kuwa hakuna vituo hewa vya kupigia kura nchini huu ni upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya viongozi wa siasa kutangaza kuwa kuna vituo hewa.

”Nashangaa kuona taarifa za uzushi zikisambaa kwenye mitandao na baadhi ya viongozi wa vyama kuanza kulalamika na kuzusha kuwa NEC imeongeza vituo hewa vya kupigia kura nchini”alisema Dk.Mahera

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here