Ndugu wa Maradona waanza kugombea utajiri

0

Buenos Aires

Ndugu wa nyota wa zamani wa soka, Diego Maradona wameanza vita ya kugombea utajiri wa Pauni 37 milioni ulioachwa na nguli huyo, ndugu wapatao 16 wametajwa katika vita hiyo.

Nyota huyo zamani wa Argentina, ambaye alifariki dunia kwa tatizo la moyo mwezi uliopita akiwa na miaka 60, hakuandika urithi wowote.

Maradona, ambaye bao lake la mkono (Mkono wa Mungu) liliimaliza England katika fainali za Kombe la Dunia 1986, alikuwa na watoto watano.

Madai hayo mazito yalianza kusikika juzi usiku katika nyumba moja iliyopo mji mkuu wa Argentina, Buenos Aires, na kuanza kuibua maswali.

Lakini watoto wengine saba wa kurithi, pamoja na wengine wanne wa kike wa Maradona, walitajwa kuwamo katika mtafaruku huo wa fedha za gwiji hilo la zamani la soka.

Chanzo cha habari kutoka Buenos Aires kililiambia gazeti la The Sun: “Vita ya kugombea utajiri wa Maradona haiwezi kutabirika, inaweza kuwa kama Kombe la Dunia.”

Taarifa za kimahakama zilibainisha kuwa Maradona aliacha fedha nchini Uswisi, Dubai na Buenos Aires, majumba karibu nchi nyingi alizotembelea pamoja na magari ya kifahari.

Katika akaunti zake pia kunaonekana kuwa na fedha zilizowekwa na kampuni alizokuwa akifanyanazo kazi kama Puma na Coca-Cola.

Maradona alidaiwa kuwa aliandika wosia 2012, lakini aliamua kuufuta kiwa madai ya kuuandika tena miaka minne baadaye.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here