Ndugai awaasa wabunge kutokuwa mabubu, watimize wajibu wao

0

Mwandishi Wetu, Dodoma

Spika wa Bunge la 12,  Job Ndugai amewaasa wabunge wasiwe bubu badala yake watimize wajibu wao.

Ndugai amesema hayo leo Jumanne  Novemba 10, 2029 muda mfupi baada ya kuapa kuwa Spika wa Bunge.

Amesema ndani ya Bunge ndiyo kunapelekwa bajeti ya Serikali, kunatungwa sheria na mipango ya Serikali, hivyo ni vema wabunge wakatimiza wajibu wao.

“Ukichagua kuwa mbunge bubu, unajipendekeza ili uonekane una nidhamu, umeliwa, ” amesema Ndugai.

Amesema siyo vema kwa mbunge kujipendekeza ili aonekane ana nidhamu kwenye chama au Serikali hatokuwa ametimiza wajibu wake wa kuwasemea wapiga kura wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here