Ndugai achaguliwa tena uspika, aizungumzia kambi rasmi ya upinzani

0

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limemchagua mbunge wa Kongwa, Job Ndugai, kuwa Spika wa Bunge la 12, baada ya kupata ushindi wa kura kwa asilimia 99.7.

Katika uchaguzi uliofanyika hii leo Novemba 10, 2020, Bungeni Dodoma, Ndugai amepigiwa kura na wabunge wateule 344 kati ya wabunge 345 na kura ya hapana ilikuwa ni moja.

Awali akiomba kura kwa wabunge hao, Ndugai amesema kuwa Bunge la 12 litakuwa ni Bunge bora na lenye mfano wa kuigwa kuliko mabunge yoyote yale na kwamba katika Bunge hilo hakutakuwa na kambi rasmi ya upinzani Bungeni kwa kuwa hawajatimiza asilimia 12.5, kwa mujibu wa kanuni za Bunge.

“Upande wa upinzani, hatutakuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani kwa kuwa hawatatimiza asilimia 12, uongozi wa spika, ofisi ya Bunge tutawatendea haki kabisa.“ amesema.

Ndugai Pia alikuwa Spika katika Bunge lililopita la 11.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here