Ndoto ya Tanzania kushiriki AFCON 2022 yazimwa na Equatorial Guinea

0

Kenya nayo yapewa mkono wa kwaheri

NA MUSSA KICHEBA

TANZANIA imetupwa nje ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kuchapwa 1-0 na wenyeji, Equatorial Guinea jana Uwanja wa Nuevo do Malabo.

Katika mchezo huo wa ‘Kundi D’ kuwania tiketi ya AFCON ya mwakani Cameroon, bao pekee la Equatorial Guinea lilifungwa na Nahodha wake, Emilio Nsue Lopez dakika ya 90.

Ndoto za Watanzania za kumuenzi Hayati Magufuli ambaye alizikwa jana, kwa kusonga mbele ziliyeyuka mbele ya vijana wa Equatorial Guinea.

Sasa Equatorial Guinea inafikisha alama tisa na kuendelea kushika nafasi ya pili nyuma ya Tunisia zote zikifuzu AFCON ya mwakani.
Tanzania inabaki nafasi ya tatu na itamenyana na Libya wiki ijayo Dar es Salaam kukamilisha ratiba.

Wakati Stars wakitolewa na kuwaacha Tunisia na Equatorial Guinea wakisonga mbele kwenye group J, wawakilishi wengine wa Afrika Mashariki Kenya nao wameyaaga mashindano hayo ya baada ya hapo jana kutoka sare ya goli 1 – 1 dhidi ya mafarao timu ya taifa ya Misri.

Goli la Mohamed Magdy limewahakikishia wa Misri kusonga mbele katika group hilo la G, na kuwaacha Harambee Stars hoi licha ya bao la Abdallah Hassan.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here