Ndoto ya Azam ni kutwaa ubingwa msimu huu- Uongozi

0

NA MWANDISHI WETU

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa  upo vizuri kwa msimu wa 2020/21 na utafanya mambo tofauti na msimu uliopita ndani ya ligi kuu bara baada ya kumaliza ikiwa nafasi ya tatu na kukosa kutwaa taji lolote lile.

Oktoba 30 ikiwa Uwanja wa Azam Complex ilikubali sare ya kufungana bao 1-1 na JKT Tanzania baada ya kutoka kupoteza mchezo wa kwanza mbele ya Mtibwa Sugar kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Jamhuri, Moro.

Ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 22 baada ya kucheza mechi 9 ikitofautiana idadi ya mabao na Yanga ambayo imefunga mabao 11 huku Azam FC ikiwa imefunga mabao 15.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ Azam FC, alisema kuwa bado wanajambo lao kwa msimu huu wana amini litatimia kwa kuwa safari ya ligi bado inaendelea.

“Bado safari ya ligi inaendelea nasi tuna kazi ya kufanya tunaamini kwamba tutafanya vizuri kwenye kusaka matokeo ndani ya uwanja kwenye mechi zetu zijazo.

“Mashabiki watupe sapoti tutafanya vizuri na hatutawaangusha katika hilo kila kitu kinawezekana kwa kuwa wachezaji wapo vizuri na benchi la ufundi lipo vizuri pia,” amesema.

Naye Kiungo wa timu hiyo, Salum Abubakar, ‘Sure Boy’ alisema kuwa ana imani kwamba kikosi hicho kitafikia malengo ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kutokana na kasi ambayo wameanza nayo.

Azam FC ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa wamecheza mechi tisa na kujiwekea kibindoni jumla ya pointi 22 na safu yao ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 15.

Kwenye mabao hayo, Sure Boy alihusika jumla kwenye mabao mawili ambapo amefunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao.

Mchezo wa kwanza kwa Azam FC ilikuwa ni mbele ya Mtibwa Sugar ilifungwa bao 1-0 baada ya kucheza mechi saba bila kupoteza na ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya JKT Tanzania Uwanja wa Azam Complex ikiwa ni sare yao ya kwanza kwa msimu wa 2020/21.

Sure Boy amesema:”Mipango ipo sawa na kila mchezaji anatambua kwamba ushindani ni mkubwa, imani yangu ni kuona kwamba kikosi kinaweza kutimiza malengo ambayo imejiwekea ikiwa ni pamoja kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.”

Mabingwa watetezi wa ligi ambao ni Simba wao wamejichimbia nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi nane ndani ya ligi na pointi zake ni 16.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here