Namungo yasonga mbele hatua ya mtoano Kombe la Shirikisho

0

  >>Yawatoa El Hilal Obed kwa jumla ya mabao 5-3  

NA MWANDISHI WETU

WAWAKILISHI wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF), Namungo FC, wamefanikiwa kusonga mbele kwenye mashindano hayo baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya El Hilal Obed, katiaka Uwanja wa Taifa nchini Sudan,

Kwa matokeo hayo Namungo FC, wanasonga mbele katika hatua ya timu 32 za mtoano kwa jumla ya mabao 5-3 ambapo katika mchezo wa kwaza uliochezwa Tanzania Namungo waliibuka na ushindi wa bao 2-0.

Pongezi zimuendee mshambuliaji Stevin Sey ambaye kwa kazi kubwa aliyoifanya Wasudan hawatamsahau.

Mchezo huo, ulianza kwa kasi huku kila upande ukielekeza mashambulizi makali kwa mpinzani wake.

Namungo walikuwa wa kwanza kupata goli la mapema kabisa, likiwekwa kimiani na mshambuji raia wa Mghana Stevun Sey.

Baada ya bao hilo, El Obed waliongeza mashabulizi na kufanikiwa kusawazisha, na dakika ya 14 wenyeji hao walirejea tena kwa kujipatia bao la pili.

Namungo ya Tanzania ilifanikiwa kusawazisha bao hilo, likifungwa na Bigirimana bleisse, kufanya mchezo huo kuwa sway a mabao 2-2.

El Hilal Obed, walifanikiwa kupata bao la tatu, ambalo hata hivyo halikudumu bada ya Namungo kusawazisha kupitia beki wake Manyama.

Hadi kipindi cha kwanza kinakamilika, kulikuwa hakuna mbabe.

Kipindi cha pili timu ziliendelea kushambuliana huku kila upande ukitafuta bao hata hvyo mabeki wa timu hizo walikuwa imara kuondosha hatari katika lango.

Hadi dakika 90 za mwaamuzi zinakamilika timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 3-3.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here