Naiona Simba SC iking’aa kwa Mkapa

0

NA MWANDISHI WETU

KUNA mudaa inabidi tujifunze kujali vya kwetu kwani ni moja ya uzalendo wa kukubali na kuthamini vya kwetu na sio vya wenzetu.

Zikiwa zimesalia siku mbili kuelekea kwenye mchezo wa marudiano ya klabu bingwa barani Afrika kati ya Simba SC dhidi ya FC Platnum ya nchini Zimbabwe huku mchezo huo ukiwa na taswira kubwa kwani atakayepoteza mchezo huo atakuwa ametolewa kwenye mashindano hayo na kwenda kwenye shirikisho moja kwa moja ikumbukwe ya kwamba mchezo wa awali Simba SC alipoteza akiwa ugenini nchini Zimbabwe kwa goli moja pekee lililofungwa na Chikwende Perfect hivyo FC Platinum wanakuja Dar es Salaam kwa Mkapa wakiwa na goli moja walililofunga wakiwa nyumbani na atakayeshinda mchezo huo atakuwa amevuka hatua hiyo na kwenda kwenye hatua ya makundi.

Namuona Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck, akifunguka zaidi kwenye mchezo huo dhidi ya FC Platnum kwa Mkapa kwani hawana cha kupoteza wanahitaji magoli mawili na zaidi ili kuwahakikishia kuendelea kusalia kwenye mashindano na kwenda hatua nyingine ya makundi ukifunguka zaidi unahitaji pia kuwa bora zaidi kwenye safu yako ya ulinzi kwani nataraji kuwaona FC Platinum wakijilinda zaidi ili kulinda goli lao na kufanya mashambulizi ya kustukiza counter attack na kwa aina ya makosa ya safu ya ulinzi ya Simba SC kwenye mechi ya awali kule Zimbabwe walinzi wake walifanya makosa ambayo yaliwaadhibu kia goli walilofungwa na kwa aina ya washambuliaji wa FC Platinum wanakasi wakiwa wanashambulia inayomlazimu mlinzi kufanya makosa na kujikuta tayari ashakosea kwenye eneo la hatari pengine kasi ya washambuliaji wa FC Platinum ndio iliwagharimu zaidi walinzi wa Simba SC kwenye mchezo wa awali kule Zimbabwe sitarajii kuona makosa yakijirudia tena kwenye ardhi ya nyumbani kwa Mkapa.

Wachezaji wanaweza kuamua matokeo wakiwa uwanjani kwa walichofundishwa na kocha lakini kocha anazoasilimia kubwa za kuamua matokeo kwa kubadilika kutokana na aina ya wapinzani wako kwa dakika 15 za awali kocha Sven ndio muamuzi mkubwa wa mchezo huu dhidi ya Fc Platnum na wachezaji wanaamua kutokana na waliyofundishwa na kocha kwa kuzingatia sychology ya wachezaji.

Mwishoni mwa wiki, uongozi wa Simba SC, ulisema kuwa wapinzani wao FC Platinum itakuwa ngumu kutoka kwenye mchezo wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Januari 6, Uwanja wa Mkapa.

Simba SC chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck ina kibarua cha kupindua meza kwenye mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ili iweze kutinga hatua ya makundi.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Haji Manara, wanatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu ila kwa namna yoyote ile itakuwa ngumu kwa wapinzani wao kutoka.

“Mashabiki wetu ambao ni mastaa namba moja ndani ya timu yetu tunawaomba wajitokeze kuipa sapoti timu yetu kwa kuwa hakuna namna mpinzani wetu hatoki pale kwa Mkapa.

“Maandalizi na mipango kuhusu mchezo wetu wa marudio yapo vizuri tunasubiri muda ufike ili tuweze kutoa burudani kwa mashabiki pamoja na kuliwakilisha taifa letu la Tanzania kimataifa,”anasema Haji Manara.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe, Simba SC ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 inakibarua cha kusaka ushindi wa mabao zaidi ya mawili ili kusonga mbele.

Tayari wapinzani wa Simba SC, FC Platinum wametia timu ndani ya ardhi ya Dar es Salaam, juzi (Januari 2 mwaka huu), ambapo wameweka wazi kwamba wamekuja kwa kazi moja ya kusaka ushindi.

IMEANDALIWA NA: FADHILA KIZIGO KOCHA MWANDISHI 0673854979 INSTRAGRAM FADHILAKIZIGO19

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here