Mzozo wa Israel na Palestina: Je kuwa na taifa moja ndio suluhisho?

0

NA MWANDISHI WETU

Israel imebuni uhusiano wa kidiplomasia na nchi kadhaa za Kiarabu ambazo hazikuwahi kuitambua kama taifa huru tangu ilipobuniwa mwaka 1948.

Muungano wa nchi za Waislamu wa dhehebu la Sunni dhidi ya Iran, Israel ikiwa kati kati ya mpango huo, umeimarishwa na baada ya ” vugu vugu la mageuzi katika nchi za Kiarabu” muongo mmoja uliyopita, uliacha demokrasia ya Tunisia mashakani.

Maandamano ya umma yamekuwa makubwa mwaka huu nchini Iraq, Algeria na Lebanon, huku vita vya wenyewe kwa wenyewe vikishuhudiwa Libya na Yemen.

Kwa upande mwingine hatu aya Urusi kuingilia mzozo wa Syria umetoa nafasi kwa rais Bashar al-Assad kusalia madarakani na kuweka wazi hatua ya kutaka Marekani kuondoka katika eneo hilo.

Kutokana na hilo, suala la Palestina, ambalo kwa miongo kadhaa limekuwa chimbuko la siasa za mashariki ya kati, limesambaratika, na kwa mujibu wa wachambuzi kadhaa suluhisho la kuwa na “nchi-mbili” limezikwa katika kabui la sahau, na wazo kwamba chaguo pekee ni kukuza jimbo lenye mataifa mawili limezinduliwa tena na wataalam wengine.

Haki ya sawa itapatikana?

 Saudi Arabia, na falme zingine za Ghuba na Misri zimeashiria kuunga mkono kubuniwa kwa taifa la Palestina,ambayo iko pamoja na Israeli, sio suala linalopaswa kupewa kipaumbele na wala hawaoni hilo ikiwezekana.

Mwanmfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman amesema – Palestina haina budi kukubali ombi la amani linalotolewa na Israel na Marekani “au wafyate mdomo.”

Mwezi Januari mwaka 2020, utawala wa Trump ulizindua mpango wa “amani na ustawi” ambao ulipingwa na mamlaka za Palestina wakidai kuwa unapendelea Israel.

Ndani ya mwaka 2020, Benjamin Netanyahu alitangaza kwamba angeongeza sehemu ya tatu ya Ukingo wa Magharibi, hatua ambayo amechelewesha, labda kutokana na mlolongo wa kutambuliwa kwa taifa la Israeli na nchi za Kiarabu.

“Wakati umewadia wa kuachana na suluhisho la kuwa na mataifa mawili na kuangazia lengo la kuwa na haki kati ya Wayahudi na Wapalestina,” mwandisi mashuhuri wa Mmarekani na Myahudi Peter Beinart aliandika katika Gazeti la New York Times mwezi Julai.

“Wakati umewadia wa kutambua nyumbani kwa Wayahudi na sio taifa la Wayahudi.”

Alisema inaweza kuwa,taifa moja linalojumuisha Israel, Ukingo wa Magharibi, Gaza na Jerusalem Mashariki, au muungano wa nchi mbili.

Ramani sita zinazoonesha maeneo ya Wapalestina imemebadilika katika miongo ya hivi karibuni.

Kwa upande wake, Gideon Levy, mchambuzi katiika gazeti la Israel la Haaretz, pia anasema “lazima tuanze kutafakari kuhusu mambo ambayo hayakuwahi kufikiriwa”, kwa sababu “hakuna njia nyingine mbadala.”

Mapendekezo la kihistoria

Pendekezo la kuwa na taifa moja la Israeli na Palestina sio jambo geni.

Mwaka 1948, mwanafilosofia Hannah Arendt alipendekeza kubuniwa kwa taifa moja linalojumuisha Wayahudi, Waarabu na makabila mengine madogo badala ya kumegua Palestina kutoka Israel.

Miongoni mwa wachambuzi hao ni, mwanasiasa wa zamani wa Israeli na mwandishi marehemu Uri Avnery aliibua wazo kama hilo mnamo 2013, kama alivyofanya marehemu Edward Said (Mpalestina) na Tony Judt (Mwingereza mwenye asili ya Kiyahudi).

Je mzozo kati ya Isarael na Palestina ulianzaje?

Mgogoro kati ya Israel na Palestina umekuwepo kwa miongo kadhaa sasa na swala la umiliki wa ardhi ndio limetajwa kuwa nyeti.

Uingereza ilichukua na kudhibiti eneo linalojulikana kama Palestine baada ya mtawala wa eneo hilo la mashariki ya kati mfalme wa Ottoman kushindwa katika vita vya duniani vya kwanza.

Ardhi hiyo ilikuwa ikimilikiwa na Wayahudi walio wachache na Waarabu walio wengi.

Uhasama baina ya makundi hayo mawili ulianza wakati jamii ya kimataifa ilipoipatia Uingereza jukumu la kuwapatia makaazi Wayahudi katika eneo la Wapalestina.

Kwa upande wa Wayahudi eneo hilo lilikuwa la mababu zao, lakini Waarabu Wapalestina pia nao walidai kumiliki ardhi hiyo na hivyobasi wakapinga mpango huo.

Kati ya mwaka 1920 na miaka ya 40, Idadi ya Wayahudi iliowasili katika eneo hilo iliongezeka, huku wengi wakitoroka kuuawa barani Ulaya na kutafuta eneo la kuishi baada ya mauaji ya Holocaust ya vita vya dunia vya WWII.

Ghasia kati ya Wayahudi na waarabu na dhidi ya utawala wa Uingereza ziliongezeka.

Mwaka 1947, Umoja wa Mataifa ulipiga kura kwa Palestina kugawanywa kati ya mataifa ya Wayahudi na Wapalestina huku mji wa Jerusalem ukiwa mji wa kimataifa.

Mpango huo ulikubaliwa na Wayahudi lakini ukakataliwa na Waarabu na haukutekelezwa.

Uanzishaji wa taifa la Israeli na ‘changamoto’ zake

Mwaka 1984 ,baada ya kishindwa kutatua mzozo huo , watawala wa Uingereza waliondoka na viongozi wa Kiyahudi wakatangaza uanzishwaji wa tiafa la Israel.

Wapalestina wengi walipinga na vitaa vikaanza.

Wanajeshi kutoka mataifa jirani ya Kiarabu walivamia. Mamia ya maelfu ya raia wa Kipalestina walitoroka ama kulazimishwa kutoka katika makaazi yao kwa kile walichokiita Al Nakba aua ‘janga’.

Wakati vita vilipoisha mwaka uliofuata , Israel ilikuwa ikidhibiti eneo kubwa.

Jordan iliteka ardhi iliojulikana baadaye kama West Bank huku Misri ikilinyakua eneo la Gaza.

Jerusalem iligawanywa kati ya wanajeshi wa Israel waliopo magharibi na wanajeshi wa Jordan waliopo mashariki.

Kwa kuwa hakukuwepo kwa mkataba wa amani – kila upande ulilaumu mwengine na kusababisha vita zaidi kwa miongo kadhaa.

(CHANZO: BBC)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here